Header Ads Widget

MSANII TOMMY WA KUTOKA NIGERIA ATUA ZANZIBAR

 

 


NA THABIT MADAI,ZANZIBAR

 

INAELEZWA Kuwa Licha ya Msukumo Mkubwa unaochagizwa na Maendeleo katika Sekta ya Sayansi na Teknolojia, Lakini Uzuri na Kiwango bora cha Mziki wa Asili Visiwani Zanzibar bado unaendelea kuwavutia Wasanii kutoka Magharib Kuja visiwani humo kujifunza na Kuimba Mziki huo.

 

Hayo yameelezwa na Msaani Maarufu wa Muziki wa  Asili kutoka Nchini Nigeria Tommy Wa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ikiwa ni mara ya kwanza kufika Visiwani humo ambapo amesema kuwa Ujio wake Umetokana na kuvutiwa kwa Mziki mzuri wa Asili Visiwani Zanzibar na Afrika ya Mashariki.

 


Amesema kwa muda Mrefu amekuwa akisikiliza Musik kutoka Afrika Mashariki hususani Tanzania na maevutiwa nao kutokakana na mpangilio wa Ala za  Musiki hivyo alitamani kutembelea katika maeneoi hayo.

 

“Kwa Muda Mrefu sana nasikiliza na kuvutiwa Musiki Mzuri kutoka Afrika ya Mashariki,Mziki Mzuri wa Asili wa Tanzania na Zanzibar hivyo nilitamani siku Moja kutembelea na kufanya Muunganiko na Wasanii kutoka Maeneo hayo,”amesema.

 

Pia ameeleza kuwa kufika kwake Visiwani Zanzibar itakuwa ni mwanzo Mzuri pamoja na kufungua fursa  kutafungua Fursa za Wasanii kutoka Zanzibar na Nigeria.

 

Katika Hatua nyingine, ameeleza adhama yake ya kufanya Mziki wa Asili ya Afrika ni kufanya Tamaduni za Afrika kujulikana Katika zaidi.

 

“Najivunia Utamaduni wangu Mzuri wa Afrika hivyo nimeamua kufanya kuimba Nyimbo za Asili za Afrika ili utamaduni wetuujulikana Nnje ya Afrika,”ameeleza.

 

Nae Mwalimu wa Sanaa na Muziki kutoka Chuo cha Muziki Zanzibar DCMA, Hassan Mahenge amesema kwamba kupata fursa ya kufanya kazi na Tommy Wa ni ataacha athari katika Muziki wa Zanzibar.

 

“Wanamuziki kutoka na Maneneo mbalimbali huwa wanaacha athari ya muziki wao pamoja kutanfaza tamaduni walizozikuta katika maeneo yao,” amefafanua.

 

Aidha ameeleza kuwa wanatamani kurekodi nyimbo na Msanii huyo kutoka Nigeria ili iwe kumbukumbu njema kwao.

 

Kwa upande wake Rais wa Taasisi ya Watu wa Utamaduni wa Afrka na Ufaransa, Mohammed Mzee amesema lengo la kumleta Msanii huyo Tommy WA Visiwani Zanzibar kutokana na aina ya Mziki mzuri wenye ladha za Afrika anaoufanya.

 

“Taasisi yetu ndio iliyomleta Tommy WA Visiwani ili kuleta chachu kwa Wasanii wengine wanaofanya Sanaa ya asili ya Afrika kama vile Taarabu, Tarajaz na hata ngoma za Asili,”ameeleza.

 

Hata hivyo Wadau Mbalimbali wa Muziki kutoka Taasisi tofauti tofauti za Sanaa na Muziki ikiwemo Sauti za Busara wamepngoza jitihada za Ubalozi wa Ufaransa na Taasisi ya Utamaduni Utamaduni wa Ufaransa Zanzibar kwa kuendelea kuleta Wasanii mbalimbali wenye athari chanya kwa Musiki wa Tanzania.

 

“Tunawapongeza kwani wanaimarisha Mahusiano na kutangaza Utamaduni wa Mzanzibar,”wameeleza.

 

Hata hivyo wametoa Wito kuwa kuendelea kuleta Wasanii hususani baada ya kipindi kigumu cha Uviko 19 kutokana na uhitaji kuburudika na kujifunza kutoka kwao.

 

Msanii Tommy WA alipata fursa ya kutoa Burudani kwa Wageni pamoja na Wazanzibar.;

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI