Header Ads Widget

WATENDAJI WA MAHAKAMA WATAHADHARISHWA DHIDI YA VITENDO VYA UVUJIFU WA MAADILI

 


Na Ibrahim Kunoga Lushoto Tanga.


Watendaji wa mahakama wametahadharishwa dhidi ya vitendo vya uvunjifu wa maadili ambavyo vinachangia kuathiri utoaji wa haki kwa wananchi kwenye maeneo yao ya kazi.


Hayo yamesemwa na msajili wa mahakama kuu ya Tanzania Wilbert Chuma wakati wa mafunzo elekeza kwa waajiriwa wapya wa mahakama ya Tanzania yaliyofanyika kwenye chuo cha mahakama cha IJA kilichopo wilayani Lushoto.



Chuma amesema mafunzo hayo yatawajenga kujifunza misingi mbalimbali ya majukumu yao ambayo yataenda sambamba na maswala ya maadili.


Amesema kazi ya mahakama Tanzania ni utoaji haki na ili haki iweze kutolewa kwa kiwango na ubora unaohitajika swala la maadili ni swala muhimu.



"Maadili ndio kiini cha haki hivyo nawasihi watumishi hawa kwa ujumla wao wanapokwenda kwenye maeneo yao ya utumishi wahakikishe wanalinda maadili ili kujiepusha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili; Amebainisha Wilbert Chuma.


Kwa upande wake Anjel Mtei ambae ni naibu katibu tume ya utumishi wa mahakama amewataka watendaji hao kujiepusha na vitendo vya rushwa vinavyoathiri utoaji wa haki.



Anjel amewataka wajitahidi kuwapa tume imani iliyopewa na tume kuthibitisha kwa vitendo kuwa tume imewaamini.


Amesema kama maadili yao hayatabadilika watapewa malalamiko kutoka kwa wananchi wanaamini wakifanya kazi kwa maadili malalamiko yatapungua na huduma ya utoaji haki yataboreka zaidi.


Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema yamewapa uelewa wa namna ambavyo wanaenda kuihudumia jamii kwenye maeneo yao ya kazi.



Mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya mafunzo ya utumishi wa umma  ya mwaka 2013 pamoja na mpango mkakati wa chuo cha uongozi wa mahakama wa mahakama Lushoto miaka mitano.


Lakini pia Sera ya mafunzo ya mahakama imeweka takwa la kufanyika mafunzo elekezi ya awali kwa kila mtumishi anayeajiriwa, kupanda cheo, au kuteuliwa kabla hajaanza majukumu mapya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI