Na WILLIUM PAUL, MOSHI.
MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro Prof. Patrick Ndakidemi amewaasa wananchi kutoa taarifa sahihi kwa mawakala wa sensa pindi muda utakapowadia ili kuisaidia Serikali kupata takwimu sahihi.
Prof. Ndakidemi alisema kuwa, Sensa inasaidia Serikali kutambua idadi ya wananchi wake na kuweza kuwahudumia kwa kuwaletea miradi mbalimbali ya maendeleo kulingana na idadi ya watu.
"Swala la umri wa mtu ni muhimu ili Serikali iweze kutambua watu wenye umri kadhaa wapo wangapi hivyo niwasisitize na kuwaomba wananchi kutodanganya katika hili" alisema Prof. Ndakidemi.
Mbunge huyo alitumia pia nafasi hiyo kuiasa jamii kutowaficha ndani watoto wenye ulemavu pamoja na wazee kwani nao ni haki yao kuhesabiwa ili waweze kuudumiwa na Serikali yao sikivu ya Rais Samia Suluhu Hasani.







0 Comments