NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera.
WATU wenye ulemavu mkoani Kagera wamejivunia kushirikishwa katika mafunzo ya makalani wa sensa ya watu na makazi inayotegemewa kufanyika Augusti 23 mwaka huu.
Hayo yamesemwa Ignas Rugemalira Laulian muwakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu wilayani Karagwe wakati akiongea na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Bukoba sekondari uliopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera baada ya kuhudhuria mafunzo ya makalani wa sensa watakwenda kusimia makalani wa sensa katika wilaya zote zinazounda mkoa wa kagera.
“Katika sensa hii itakayofanyika Augusti 23 kwetu tunaona imekuwa shirikishi kwa sababu viongozi wetu wametushirikisha vya kutosha kwa umoja wetu ili kutoa elimu ya juu ya umuhimu wa sensa hasa kwa wananchi wakiwemo watu wenye ulemavu, tupo wawakilishi kutoka vyama vya wasioona na makundi yote yameletwa katika mafunzo haya”
Ameongeza kuwa kupitia ushirikishwaji huo viongozi wa watu wenye ulemavu wamenufaika sana hasa kujua umhimu wa zoezi la sensa kwa watu wenye ulemavu huku akiahidi kuwa watakuwa mabalozi wa kuwaamasisha wenzao watakaporudi katika maeneo yao wajitokeze kuhesabibwa ifikapo August 23 mwaka huu.
Naye mkufunzi wa sensa Kitaifa, Boneventura Angelo Mshongi amesema kuwa wanaendelea kuwafundisha makalani ambao wataenda kuwafundisha makalani katika wilaya huku akisema kuwa ukusanyaji wa taarifa utafanyika kidigitali.
“Sensa ya mwaka huu itakuwa ya kitofauti sio kama tulivyokuwa tumezoea, itanyika kitekinolojia zaidi kidigitali kwa kutumia vifaa maalumu kama vile vishikwambi hatutumii karatasi kama tulizokuwa tunatumia na hii itasaidia ufanikisha upatikanaji wa data zote na zenye usahihi” alisema Mshongi.
Lucy Emily ambaye ni miongoni mwa mkufunzi wa sensa watarajiwa watakaoenda kufundisha makalani kwa ngazi ya wilaya amesema kuwa kutokana na mafunzo waliyopata yamesaidia kuongeza uelewa hasa juu ya matumizi ya vifaa vitakavyo tumika kukusanya data na huku akisema kuwa wawafundisha vyema makalani ngazi ya wilaya ili kusaidia upatikanaji wa data zilizo sahihi.








0 Comments