Madaktari bingwa watatu wa magonjwa mbalimbali kutoa nchini Korea wakishirikiana na madaktari 9 kutoka Mkoa wa Mwanza wamepiga kambi kutoa huduma za afya bure kwa wananchi waonakaa visiwa vilivyoko wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza.Na MatukioDaimaApp Mwanza
MATHEW LUBONGEJA makam wa rais wa shirika hilo lisilokuwa la kiserikali kutoka nchini korea amewasihi wananchi wote kujitokeza kupata hudum hiyo.
pia ameishukuruku serikali ya rais samia na ofisi ya mkuu wa mkoa wa mwanza kwa kuwapa ushirikiano tangu wamefika nchini na wakiendelea kutoa huduma kwa wananchi wanaoishi katika viziwa vya ziwa victoria
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Buchosa, Dk Deus Dakama amesema huduma hizo zimeanza jana kisiwani Kome kambi ya uvuvi ya Kome Mchangani inayotolewa bure na madaktari hao wakishirikiana na madaktari Wakitanzania.
madaktari hao wakishirikiana na madaktari Wakitanzania.
Amesema wananchi wa maeneo hayo watapata huduma bure za vipimo na dawa kwa yoyote atayekutwa na ugonjwa.
DK Dakama amesema kwenye kambi ya uvuvi ya kome mchangani walipima zaidi ya 300 na ugonjwa kubwa uliobainika kuwakabili wakazi wa maeneo hayo ni shinikizo la damu na Kichocho kutokana na wakazi hao kutumia maji yasiyosafi na salama.
" Jana tulianza mchangani Leo tuko Ntama tunatia huduma bure za afya kwa wananchi hivyo wananchi wanatakiwa kutojitoza kwangi kupata huduma hiyo "amesema Dk Dakama.
Juma Hasani mmoja wa wakazi wa Kome Mchangani amesema wameridhishwa na matibabu yanayotolewa na madaktari kutoka Korea wakishirikiana na madaktari kutoka Tanzania.
Huduma hiyo inatolewa na madaktari hayo kutoka Korea wanaotokana na Shirika la Kimataifa la Christian Life World Mission Frontiers yenye makazi yake nchini Korea.












0 Comments