NA: FRANCO NKYANDWALE MATUKIO DAIMA APP SUMBAWANGA.
Kadri maandalizi ya mashindano ya michezo ya UMISETA inavyo shika kasi nchini na kwenye viwanja vya ITWELELE sekondari katika Halimashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Kapteni wa timu ya ITWELELE sekondari Godfrey amesema hayo leo.
Kapteni Godfrey alisema mara nyingi Shule hukosa mipira ya kufanyia mazoezi ila wakati wa mashindano yanapo karibia ndipo wanafunzi huanza kufanya mazoezi kwa kasi na kuingia kwenye USHINDANI kwa kutumia mipira michache kwa wavulana na wasichana na hawana viatu na wakati mwingine wanashughulika na vipindi ya darasani zaidi.
Pamoja na ushindi mwembamba wa goli moja wa timu ya ITWELELE sekondari dhidi ya Shule ya USHINDI sekondari baada ya dakika 90 goli ambalo lilipatikana katika kipindi cha pili, goli lilifungwa na Gizibert Kazule aliyecheza namba Tisa.
Katika mchezo wa Mpira wa miguu kwa wasichana wa Shule hizo timu zote zilitoka suluhu kwa goli moja moja, timu ya USHINDI ilifungua lango la ITWELELE katika kipindi cha kwanza kwa mkwaju uliopigwa na Anjelina ambapo timu ya ITWELELE sekondari ilisawazisha katika dakika za majeruhi za kipindi cha pili, namba nane Lucy alipowapiga chenga beki na golikipa wake.









0 Comments