Header Ads Widget

WAZAZI MSIFICHE WATOTO WENYE ULEMAVU NDANI -MBUNGE FYANDOMO.


Na Matukio daima media , Mbeya

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Suma Fyandomo amewahamasisha wazazi na walezi kutowaficha ndani watoto wenye Ulemavu ambao wamefikia umri wa kuanza masomo.


 


Fyandomo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na matukio daima  kuhusiana na wazazi ambao wamekuwa wakificha watoto ndani kwa kuogopa kuchekwa na jamii inayowazunguka.


 


Fyandomo amesema  kuwa wanawake walio wengi wakizaa watoto wenye ulemavu wanakuwa hawako tayari  kuwapokea hao watoto lakini kwasababu anakuwa amembeba miezi tisa tumboni  inabidi aendelee kumtunza lakini katika kumtunza kwake anakuwa anamficha ndani hivyo mtoto  huyo anakosa haki zake  elimu na haki zingine za msingi kama  walivyo watoto wengine .


 


“Wapo wanaume ambao wanawatelekeza wake zao sababu amezaa mtoto mwenye ulemavu hii si tabia njema ,lakini Mwanamke nae anakuwa  hayuko tayari kulikubali hili lakini kwasababu amembeba mtoto huyo miezi tisa  na anakuwa na uchungu nae hivyo katika kumtunza kwake anamficha ndani”amesema  Mbunge huyo.


 


Aidha Mbunge huyo amewasaa wanawake wa mkoa wa Mbeya kuwatoa watoto ndani wenye ulemavu kwani  kuna shule ya  watoto  wenye ulemavu ipo mkoa wa Mbeya wilaya ya Rungwe kata ya Lubiga ipo vizuri inawalea vizuri watoto na wanapata elimu nzuri  kwani shule hiyo ni ya serikali na hakuna grama zozote .


 


Hata hivyo amesema  kuna viongozi wakubwa ni walemavu ya mkini hao watoto wanaofichwa wakaja kuwa viongozi wakubwa lakini mzazi anaona njia sahihi ni kumficha mtoto ndani ili kukwepa aibu kwa jamii .


 


“Kujifungua mtoto mwenye ulemavu ni bahati mbaya tu na ni mapenzi ya Mungu  kwasababu mlemavu ni binadamu inatakiwa kupata haki zake za msingi  ,anatakiwa kupelekwa shule na kupatiwa mahitaji yake yote tunawahitaji watu wenye ulemavu ni wenzetu na tunawajali na` serikali inawajali “amesema Fyandomo.


 


Naomi Juma ni mkazi Simambwe wilaya ya Mbeya amesema kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa wakificha watoto wao wenye ulemavu ndani kutokanana kuogopa kuchekwa na jamii na wengi wanashindwa kuikubali ya kuzaa mtoto mwenye ulemavu hivyo badala yake huamua kumficha ndani ili asiweze kujulikana na mtu yeyote. 


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dkt. Vicent Anney amesema ameagiza kwa maafisa maendeleo ya jamii wilaya  na wenyeviti wa vitongoji na maafisa watendaji kupata orodha ya watoto wenye ulemavu waliopo katika wilaya hiyo 




 Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI