Wananchi Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, wameshauriwa kujijengea tabia za kula vyakula vya asili ambavyo vitasaidia kuepuka kupata Magonjwa yaliyoambukizwa ambayo hutumia gharama kubwa kuwajibu.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya hiyo Itikija Msuya ametoa ushauri huo Wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji Magonjwa yasiyo ambukiza uliofanyika katika Hospital hiyo,kwa ufadhili wa Al Ata'a pamoja na Qatar Charity kutoka Dar esalamu Kwa kushirikiana na BAKWATA Mkoa Kilimanjaro.
Alifafanua kuwa Magonjwa yasiyoambukizwa yameongezeka kwa kutokana na kuacha kutumia vyakula vya asili ambavyo vilikuwa vikisaidia kuongeza vitamin ,Protini pamoja na madini mwilini.
Msuya amesema katika kipindi cha Junuari hadi June mwaka huu,katika Wagonjwa ambao wamewaona kwenye idara ya Wagonjwa wa nje katika Halmashari hiyo asilimia 13 ya Wagonjwa hao ni Magonjwa yasiyo ambukiza yakiwamo Presha na Sukari
Amesema katika kipindi hicho cha miezi sita inaonekana Watu wengi wana shida ya Presha ni wengi sana wakifuatiwa na Watu wenye tatizo la Sukari
Ambapo katika ,ushauri wake amesema ,kitu cha Kwanza na cha Msingi zaidi tunapenda kuzuia Magonjwa yasitokee , Magonjwa haya yanaweza kuzuilika kwa kula vyakula vya asili na kufanya mazoezi
"Ni kweli ili Magonjwa haya yasiendee kuongezeka Wananchi watumie chakula vya asili na kufanya mazoezi na usipofanya hivyo utajikuta umepata Magonjwa hayo na kuanza kutumia fedha nyinyi kujitibu na pia nguvu kazi ya Taifa kupunguza kutokana na Watu wengi kuwa na Magonjwa hayo"amesema Msuya
Mkurungenzi wa Taasisi hiyo Ahmad Hamrawy,,amesema taasisi imejikita katika mswala ya kijamii ikiwamo Afya ,hivyo kuahidi kuendelee kusaidia Wananchi ,ambapo amesema katika kutoa huduma ya Afya wamekenda Mikoa Mingi ikiwamo Kigoma,Arusha na Kilimanjaro,kwa hapa Wilaya ya Hai wanatarajia kutoa huduma ya kupima Afya na kutoa Dawa bure kwa Wananchi 500
Mkuu wa Wilaya hiyo Juma Irando ,ameipongeza taasisi hiyo kwa Kuona umuhimu wa kusaidia Wananchi kuwapatia huduma bure,naomba taasisi nyingine ziiga uugwana huu.







0 Comments