Na MatukioDaimaAPP, Dar es salaam
Watanzania wameshauriwa kuanza kutumia mashine ya kukamua mafuta ya Nazi ili kutunza ubora na kuondokana na harufu inayotokana na mafuta hayo kuchemshwa kwenye moto.
Akizungumza wakati wa maonyesho ya sabasba saba mtafiti wa zao hili kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania Tari kituo cha mikocheni Violet Kiwia alisema mafuta yanayokamuliwa yanaweza kutumika hadi kwenye kupikia chakula.
“Sisi tunajukumu la kuangalia zao la nazi ambalo kwa wingi linalimwa mikoa ya pwani ambapo tuna kitengo cha kuzalisha mafuta ya nazi ambayo yanatengenezwa kwa teknolojia mpya ambayo inatengeneza mafuta bila kuyapika ambapo yakichemshwa kuna baadhi ya viini lishe visivyorafiki na joto vimekuwa vikipotea”
“Sisi tunayoteknolojia mpya ya kutengeneza mafuta bila kuchemsha ni mazuri meupe hayana harufu yanaweza kutumika kwa motto aliyezaliwa leo mpaka mtu mzima hata mtu awe karibu na ww hawezi sikia harufu unaweza pia kutumia kwakupikia kwenye chakula ambapo kunakuwa na viiini lishe vyote ni mafuta mazuri”
“Tunapotoa mafuta yanabaki machicha hayo yanaweza kutumka kwenye kuchanganga na unga lishe, chakula cha mifugo ama viwandani kwenye pipi ama biskuti na kwa baadhi ya mikoa wameshaanza kutumia teknoloji na hii kama vile Tanga, Mtwara na Lindi”
“Tunawakaribisha wawekezaji wafanyabishara vikundi ili waijue hii teknolojia nzuri ambayo wanaweza kuanza kuitumia" alisema Kiwia
0 Comments