Na MatukioDaimaAPP, Dar es salaam
Wakulima wa zao la mahindi nchini wameshauriwa kulima zao hilo kwakutimia mbegu bora zilizofanywa utafiti na Tari Tumbi ili kuongeza tija na manufaa kwenye kilimo.
Akizungumza katika maonyesho ya Sabasaba Mtafiti wa mzao ya Mahindi na Mtama kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanznaia Tari kituo cha Tumbi Tabora Dr John Libulu alisema zipo aina tatu za mahindi ambazo zinamavuno mengi na kuvumilia ukame hivyo kuleta tija kwa wakulima wa zao hilo.
“Tunazo mbegu za uchavushaji huru OPV aina mbili mpya ambazo t104 tani nne na nusu kwa hekta sawa gunia 18 -20 tofauti na mbegu za asili ambazo wanapata tani 2-3 wastani wa gunia 4-5 kwa hekari”
“Ipo pia T105 inatoa tani 5 nanusu sawa na gunia 20-22 zenye kilo 100 na aina ya tatu ni zile chotara th501 ambayo inazalisha gunia 24-30 kwa hekari tani 6 hadi sita na nusu zina uwezo mkubwa wa kutoa mavuno kwa wingi” alisema Dr Lobulu
MWISHO
0 Comments