Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma limepongezwa kwa upanuzi na ukarabati wa kituo cha afya kilichojenga kwa gharama ya mapamto yao ya ndani huku akibainisha kwakufanya hivyo wamezingatia uzalendo wa nchi.
Hayo yalisemwa Jijini Dodoma na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Kabir Shekimweri alipokuwa akizungumza na watoa huduma na wagonjwa waliokija kupata matibabu katika kituo hicho Wakati akizundua jengo hilo la utawala la kituo hicho cha afya cha polisi Dodoma.
Alisema Zahanati hiyo ilianzishwa muda mrefu tangu Miaka ya 80 na mwaka 2011 ilipandishwa hadhi na kuwa kituo Cha afya lakini bado ilikuwa miundombinu hafifu.
"Niwapongeze Jeshi la Polisi kupitia uchangiaji wa michango ya bima ya Afya mmeweza kujibana kwa mapato ya ndani na kufanya upanuzi kwa jengo hili la utawala," Alisema Shekimweri
Aliongeza Kusema "Nawapongeza kipekee sio tu Kwa ujenzi huo wa jengo hilo la kiutawala lakini kwa ujenzi unaoendana na thamani ya shilingi milioni 30.1 ikiwa na usawa wa mradi huo mmeonyesha uzalendo kwani mmefanya kazi hiyo kwa umakini bila wizi wowote," Alisema Mkuu huyo.
Aidha aliwaasa wananchi wa mkoa was Dodoma kujitokeza kwa wingi kupata huduma za Afya zinazotolewa katika kituo hicho Kwa kampeni ya afya bomba.
Hata hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi Agosti 23 na Kutoa ushirikiano katika zoezi la Sensa ya Watu na makazi.
" Kwakufanya hivyo mtaisaidia Serikali kupata idadi kamili za takwimu zinazotakiwa kuleta Maendeleo kwa jamii," Alisema Shekimweri
0 Comments