Header Ads Widget

MBIO ZA MARATHON JUMUIYA YA MADOLA KURINDIMA ASIBUHI HII BIRMINGHAM, SIMBU KUONGOZA MASHAMBULIAJI

 

Wakimbiaji wa mbio fupi na za kati wakiwa tayari kuwasaidia wenzao sehemu ya kuanzia mbio za Marathon alfajiri ya leo jijini Birmingham, Uingereza


Tanzania leo inatupa kete za kwanza katika riadha Michezo ya Jumuiya ya Madola wakati wanariadha wanne wa mbio ndefu (Marathon) wanawake na wanaume wakichuana asubuhi hii.


Wanariadha hao wa marathon ni Alphonce Simbu, Hamisi Misai, Jakline Sakilu na Failuna Matanga.


Kwenye michezo hiyo Tanzania inawakilishwa na wanariadha tisa, mabondia watatu, wacheza judo wawili, waogeleaji wawili na mnyanyua vitu vizito kwa walemavu (Para-Powerlifting) mmoja.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI