MKUU wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi mapema leo amepokea na kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru, pamoja msafara wa wakimbiza mwenge kitaifa, kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Conl. Denis Mwila
Katika makabidhiano hayo, Mhe. Makilagi amebainisha Mbio za Mwenge wa Uhuru zitapita katika maeneo mbalimbali katika kata zote sita za wilaya hiyo, zinazojumuisha takribani Kilomita 24.3.
Aidha, amesema mwenge Uhuru unatarajia kukagua, kuzindua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo katika huduma za jamii, yenye thamani ya Tsh. 5 Bill.













0 Comments