SERIKALI imewaasa na kuwataka wafugaji nchini kufanya shughuli hiyo Kwa njia za kisiasa zaidi, ili kujiletea tija na manufaa mfambuka kiuchumi.
Ushauri huo umetolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Mashauri Ndaki (Mb), wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maonesho ya Mifugo Kibiashara ( MMK), katika viwanja vya Highland Estates Ltd., Ubena- Zomozi, Chalinze mkoani Pwani.
"Ni lazima wafugaji tubadishe mifumo na njia za kuendesha shughuli zetu, ni muhimu sasa kutumia njia za kisasa zaidi, ikiwa ni pamoja na kutumia mbinu, ujuzi na maelekezo kutoka Kwa wataalamu wetu waliopo katika meneo yetu, " alisema Mhe. Ndaki.
Aidha, Ndaki ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Maswa-Magharibi (Mkoani Shinyanga), ameonya baadhi ya wafugaji kutumia njia za kienyeji pamoja na Imani za asili katika kuendesha shughuli za ufugaji
Katika hagla hiyo, ambayo pia ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Abdallah Ullega (Mb), ilitoa mwamko na morali Kwa wafugaji kutumia mbinu za kisasa zaidi.







0 Comments