NA MATUKIO DAIMAAPP,KAGERA
BAADHI ya wafugaji katika Wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera wamelalamikia ufinyu wa maene ya malisho, jambo linalopelekea kuibuka Kwa migogoro ya mara kwa mara, baina yao na wakulima pamoja na Mamla ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA).
Wakiwasilisha shida na adha wanazozipata katika shughuli zao mbele ya Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi, Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa, wafugaji hao wamebainisha ongezeko la mifugo linaloelemea maeneo yaliyopo, linapelekea baadhi ya mifugo kuvuka mipaka na kuingia kwenye mashamba ya mazao ya chakula, pamoja na maeneo ya Hifadhi za Taifa, mapori tengefu na misitu hali inayochangia kuibuka Kwa migogoro baina yao na wakulima, pamoja na kuchukukiwa sheria na mamlaka za uhifadhi, ikiwemo Wakala wa Misitu (TFS).
Akijibu malalamiko hayo, mbunge huyo amesema amekwishafikisha jambo hilo Kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kupitia Naibu Waziri wake, Mhe. Abdallah Ullega (Mb), ambaye aliahidi jambo hilo lipo katika hatua za utatuzi.
Kuhusu Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe. Chiwelesa alisema analibeba na kwenda kuonana na wahusika wizarani, ili kuona namna ya kutatua jambo hilo na kuwaondolea adha wafugaji hao huku akisisitiza kutawala Kwa amani kati ya wafugaji na wakulima wilayani humo.
Baadhi ya wafugaji wakiwa katika mkutano na mbunge wa Biharamulo mhandisi Ezra Chiwelesa








0 Comments