NA HADIJA OMARY MATUKIODAIMA APP _LINDI……….
KUTOKANA ongezeko la kasi ya teknolojia Duniani ambapo imefanya Benk nyingi kuwa wabunifu katika kuangalia namna bora na mzuri ya kuweza kuhudumia wateja wake Bank ya NMB kanda ya kusini imezindua kampeni ya NMB teleza kidijitali ili imeboresha Teknolojia..
Uzinduzi huo wa NMB Teleza kidijitali uliofanyika katika uwanja wa michezo wa Chuo cha ufundi Stadi (VETA) Mkoani Lindi ulienda sambamba na bonanza la michezo mbali mbali pamoja na uzinduzi wa klabu mbili za Bank hiyo kwa wanafunzi wa chou wenyeji (VETA) na chuo cha Lindi college of helth and Allied science (LICHAS).
Akizindua kampeni hiyo Meneja wa NMB Kanda ya Kusini BI. Janeth Shango Alisema kadri Teknolojia inavyozidi kuwa kubwa inazidi kurahisisha maswala mbali mbali katika utendaji wao wa kazi na Maisha ya kila siku ambapo katika utendaji wa Maisha ya kila siku endapo utakuwa na teknolojia mzuri kazi zako zitakuwa rahisi .
Kuhusu kampeni hiyo ya Teleza kidigitali Bi Shango alisema Benk hiyo umekuja na huduma tatu ambazo ni mshiko fasta unaomuwezesha mteja wa NMB kuweza kukopa mikopo midogo midogo hadi kufikia shilingi laki tano kwa kutumia huduma ya NMB mkononi kupitia simu yake pasipo kuhitaji kujaza fomu ya maombi ya mkopo
“Leo hii tumeona kuna wale ambao watamaliza chou, unafika Mtaani unategemea pengine unahitaji mtaji wa laki tatu tu , unao uwezo wa kokopa mtaji wa laki tatu kupitia simu yako, na ukafanya unachokihitaji ukawa Tajiri mkubwa katika siku za baadae” alisema
Aliitaja huduma nyingine atakayoipata Mteja kupitia Mpango huo ni NMB Pesa Wakala, katika huduma hii mteja anao uwezo wa kupata huduma za kutoa ama kutuma pesa kupitia simu yake iliyounganishwa na NMB mkononi kwa wakala yeyote wa Bank hiyo bila kuwa na kadi.
Huduma nyingine ya tatu kupitia kampeni hiyo ya teleza kidigital ni NMB lipa mkononi ambapo mteja hatakuwa na sababu ya kutembea na pesa mkononi kwa ajili ya kufanya matumizi mbali mbali ya mahitaji yake bali kupitia simu yake anaweza kupata huduma yoyote kupitia mfanyabiashara aliejisajili na hudama hiyo
“Nyinyi ni vijana na vijana wa leo hawatembei na pesa mkononi bali wanatembea na kadi au na simu ukifika pale kwa mangi unataka kununua mahitaji yako yawe yoyote unaouwezo wa kulipa kwa kupitia simu yako tu” alieleza
Pamoja na mambo mengine Bi. Janeth alitumia fursa hiyo kuwataka wanachuo hao pamoja na wafanya biashara wadogo , wakati na wakubwa kuchangamkia huduama hizo za NMB teleza kidijitali ili kuweza kupata huduma kwa haraka na kwa wepesi Zaidi.
Kwa upande wake Twahiba Shabani Mwanafunzi wa Chuo cha Ufundi VETA alisema kuwa Uwanzishwaji wa klabu hizo umewapa nafasi pana Zaidi wao kama wanachuo kushirikiana na Bank hiyo ya NMB katika kujifunza maswala mbali mbali ya kifedha ikiwemo kuweka Akiba
“Kupitia uzinduzi huu wa NMB teleza Kidigitali sisi imetusaidia sana kwa sababu wanachuo tuliowengi tulikuwa hatua Elimu ya Kifedha hivyo kupitia kampeni hii tumejifunza mambo mengi pamoja na kutupa fursa ya kufungua Akaunt za Kibenk” alisema Twahiba
0 Comments