Header Ads Widget

WAFANYABIASHARA WAPEWA ELIMU JINSI YA KUSIMAMIA BIASHARA ZAO

 



Wafanyabiashara mbalimbali mkoani Kilimanjaro wamepewa elimu juu ya jinsi ya kisimamia biashara zao na jinsi ya kukabiliana na changamoto Zilizopo katika biashara zao.


Akizungumza katika warsha hiyo meneja wa benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Dusmass Prosper amesema kuwa wamekuwa wakikutana na wafanyabiashara Kila mara na kiwapa elimu ambayo imeonesha kuongeza tija kwa wafanyabiashara na wao wamekuwa wakipata nafuu kwani wanafanya kazi na watu ambao tayari Wana uelewa  na umuhimu wa kutumia benki katika biashara zao.


Aidha amesema kuwa mategemeo ya benki ni kwamba wanapotoa mafunzo hayo wafanyabiashara hao  wataenda kufanya biashara  wakiwa na elimu ya kutosha itakayowasaidia kuweka mipango na mikakati katika kukuza biashara.



Kwa upande wake Virginia Silayo mwenyekiti wa NMB Business Club mkoa wa Kilimanjaro amesema kuwa kukutana kwa wafanyabiashara hao kutasaidi kitambua changamoto zinazoikabili na jinsi ya kuweza kuzitatua .


Pia Amesema kuwa  Klabu hiyo ya NMB Business club itasaidia kuboresha mahusino ya wafanyabiashara na wananchi pamoja na tasisi za kiserikali zinazotoa huduma kwani wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali watakutana na kupeana ujuzi.


 Amewataka wafanyabiashara kuangalia Serikali inataka Nini ili na taratibu zipi za Serikali zinazotakiwa kizifuata ili kuimarisha biashara.



Akitoa elimu ya juu ya umuhimu wa kulipa Kodi Afisa mahusiano na elimu kwa  mlipa Kodi mkoa wa Kilimanjaro TRA Ndugu. Odupai Papa amewataka wafanyabiashara kifuata Sheria Kama kutaonekana Kuna Sheria itakayowabana.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI