Header Ads Widget

WACHEZESHA KAMARI NJOMBE KUSAKWA

 



Na Gabriel Kilamlya, MATUKIODAIMA APP NJOMBE


Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe  Lauteri Kanoni ametangaza kuanzisha msako mkali wilayani humo ili kuwakamata wafanyabiashara wanaochezesha mchezo wa kamari kupitia mashine zilizosambaa kila mahali na kusababisha wakulima kulazimika kuuza chakula cha akiba walichonacho ili wapate Fedha za kucheza kamali.


Amesema hayo Wakati Akitoa Wito Kwa Maafisa kilimo 36 kutoka kila kata ambao wamekabidhiwa usafiri wa pikipiki uliotolewa na serikali kwa ajili ya kuwawezesha kutumia taaluma walizo nazo kutoa elimu kwa mkulima ili aweze kufanya kilimo chenye tija na kuwasisitiza maafisa kilimo hao kuwa moja ya jukumu walilonalo hivi sasa ni kuwaelimisha wananchi na wakulima kutunza chakula walichonacho badala ya kuuza chote.


Kanoni Amesema Katika Wilaya ya Wanging'ombe Zipo Mashine za Michezo ya Kamali zaidi ya 100 Ambazo Zinasababisha Wananchi Kuuza Mazao Yao na Kwenda Kuchezea Kamali Jambo Ambalo ni Hatari Kubwa Ukizingatia Kumekuwapo Kwa Uhaba Mkubwa wa Mvua Mwaka Huu.


Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe, Bi. Mariam Muhaji amesema hatarajii kuona matumizi ya pikipiki hizo aina ya Boxer zinafanya kazi nje ya lengo lililokusudiwa.


Kwa Upande wao Maafisa Kilimo waliokabidhiwa pikipiki hizo akiwemo Francista Niseli na Benaderta Selestine Wamesema Wanatarajia Kwenda Kufanyakazi ya Kuwatembelea Wakulima na Kuwapa Elimu Kikamilifu.


Wataalamu Mbalimbali wa Kilimo Nchini Wamekabidhiwa Pikipiki Hizo Kwa ajili ya Kwenda Kutoa Huduma Bora za Ugani Kwa Wakulima.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI