Header Ads Widget

WAFANYABIASHARA MWANZA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIBENKI

 


Na Mwandishi wetu_Mwanza.


Mkuu wa Mkoa  wa Mwanza Mhandishi Robert Gabriel amewataka  wafanyabiashara wa Mwanza kutumia vizuri fursa mbalimbali wanazopewa na banki ya NBC .kwani zina manufaa makubwa kwenye kukuza  biashara Nchini.


"Banki ya NBC ni benki kongwe na ya serikali ambayo kimsingi inatoa huduma mbalimbali za kibiashara, hivyo wafanyabishara wa Mwanza wajitokeze kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye banki ya NBC". Alisema Mhandishi Gabriel.


Vile vile Gabriel alitoa wito kwa banki ya NBC kujikita kwenye kutoa elimu kwa umma ili jamii ielewe umuhimu wa kuweka akiba katika maisha na uwekezaji kwani jambo hilo ni muhimu sana.




 Mkurugenzi wa idara ya wafanyabiashara wakubwa NBC makao makuu James Meitaron  alisema benki ya NBC ina huduma mbalimbali za  ukopeshaji bila dhamana ikiwemo wale  waliopata tenda toka Serikalini za kutekeleza miradi ya kimaendeleo kama ujenzi wa barabara.


Pia alieleza kuwa, NBC wamekuwa wabia wa maendeleo ndio maana wanadhamini ligi kuu ya NBC  na mambo mengine.


Bwana  metro akisema kuwa kwa upande wa wafanyabiashara wadogo nao  inawajali  kwani kuna huduma maalumu za mikopo kwa wafanyabiashara wadogo na wakati.




Meneja wa NBC Mwanza Thomas Lijaji alisema kuwa, benki ya NBC ina malengo makubwa ya kuwafikia watanzania wengi ili waweze kunufaika na fursa za NBC


Benki ya NBC iliandaa hafla ya jioni kwa wateja wake wote wa Mkoa wa Mwanza ikiwa na lengo la kuwashukuru wateja wake na pia kueleza fursa mbalimbali zinazotolewa  na benki hiyo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI