Header Ads Widget

SERIKALI MKOANI KAGERA YA DHAMIRIA KUIMARISHA HUDUMA YA VYOO KWA WAKAZI WAKE.

 


NA TITUS MWOMBEKI, MATUKIODAIMA APP KAGERA


Serikali mkoani Kagera imedhamiria kuimarisha huduma ya vyoo kwa wakazi wa mkoa huo ili kuwanusuru wananchi wake dhidi ya magonjwa yatokanayo na uchafu.


Hayo yamesemwa na afisa afya mkoa wa Kagera, Zabroni Segeru wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ili kuwaeleza jinsi serikali ilivyojipanga kuamasisha wananchi wake  kujua umuhimu wa kuimalisha huduma ya vyoo ili kupunguza magonjwa yatokanayo na uchafu  mkoani humo na kusema kuwa kati ya magonjwa makuu yanayosumbua wananchi hao kubwa ni yale yatokanayo na uchafu.


"Tunategemea kuanza kutembea mtaa kwa mtaa ili wananchi waweze kutambua umuhimu wa huduma ya vyoo bora, hii ni baada ya kugundua kuwa kaya 99.5 ndizo zenye vyoo bora na 0.5 bado hazijawa na vyoo bora suala linalopelekea wananchi wengi kusumbuliwa na magonjwa yatokanayo na uchafu kama vile kipindupindu"


Ameongeza kuwa, sheria zipo zinazoita kila kaya kuwa na choo bora hivyo wananchi wanatakiwa kuifuata kwa kuwa na vyoo bora kwa kila kaya ili kuepusha adhabu ambayo itatolewa wale wote watakaokahidi sheria hiyo.


"Sheria zipo wazi wananchi wanapaswa kuzifuata ili kuepusha hatua kali zitakazochukuliwa dhidi ya wale wote watakaokahidi kuwa na choo bora, tunawaomba pia wadau mbalimbali pamoja na serikali za mitaa na vijiji kushirikiana na serikali kuhamasisha wananchi kujua umuhimu wa choo bora" alisema Segeru.


Kwa upande wake Anold Kailembo mkazi wa kata ya Bakoba iliyopo manispaa ya Bukoba ameishukuru serikali kwa kutambua umuhimu wa kuamashisha wananchi kujua umuhimu wa kuwa na choo bora ili kuwanusuru wananchi dhidi ya magonjwa yatokanayo na uchafu.


"Wananchi wengi hawajuhi umuhimu wa kuwa na choo bora hii ni kutokana ukosefu wa elimu, sisi watu tunaoishi mlimani unaangaika sana watu hawana vyoo na wengine wanatapisha vyoo hovyo muda wa mvua uchafu wote unaishia kwenye vyanzo vya maji suala ambalo linapelekea wananchi kuugua magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu"


Aiomba serikali kuendelea kutoa elimu sio kutoa siku moja na kuishia pale na hii itasaidia kubaini wale wote wanaokiuka maagizo ya kuwa choo bora suala linalopelekea kudhoofisha nguvu kazi ya taifa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI