Na Gabriel Kilamlya NJOMBE
Mapokea Makubwa ya Elimu ya Uzazi wa Mpango Kwa Wakazi wa Kijiji Cha Kisilo Kata ya Lugenge Mkoani Njombe Kumetajwa Kuathiri Ongezeko la Watu Kutokana na Mabadiliko ya Kimwili Yaliyosababisha Vijana Wengi wa Kike Kuwakosesha Uwezo wa Kuzaa Kutokana na Mabadiliko ya Kimwili baada ya Mpango Huo.
Uzazi Huo wa Mpango Umeripotiwa Kukwamisha Ongezeko la Watu Kwani Kijiji Hicho Kimeonekana Kutokuwa na Watu Wengi hadi Kusababisha Shule yao ya Msingi Kuwa na Idadi Ndogo ya Wanafunzi Licha ya Kujengwa Kwa Miundombinu Mingi ya Shule.
Diwani wa Kata ya Lugenge Philoteus Mligo Akiwa Katika Mkutano wa Hadhara Kijijini Hapo Anatumia Fursa Hiyo Kuhamasisha Jamii Kuongeza Kasi ya Kuzaliana Kwani Amekuwa Akisemwa na Viongozi Wenzie.
Sanjari na Hilo Diwani Mligo Anakemea pia Tabia Iliyojengeka Kijijini Hapo ya Kutaka Kuoana Toka Ndani ya Kijiji Kwani Inasababisha Kuanza Kuoana Katika Koo Moja.
Kituo Hiki Kimelazimika Kufanya Mazungumzo na Wakazi wa Kijiji Cha Kisilo Kujua Undani wa Suala Hilo Ambapo Baadhi Yao Akiwemo Max Ngailo,Jonesia Nziku na Frank Ngailo ,Wanasema Licha ya Kuwapo Kwa Hali Hiyo Lakini Ugumu wa Maisha Pia Unasababisha Kutoongeza Familia.
Hata Hivyo Wakazi Hawa Wanakiri Kuwapo Kwa Mabadilo ya Mila za Kuoana Ndani ya Kijiji na Kwamba Hivi Sasa Vijana Wanakwenda Kuolea Mikoa ya Mbali Tofauti na Hapo Awali.
0 Comments