Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linachunguza chanzo cha ajali iliyotokea katika Barabara ya Tinde-Shinyanga na kusababisha kifo cha mwendesha bodaboda anayeitwa ASHRAF LUHUNZI mkazi wa Mbuyuni kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga.
Katika taarifa yake kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishna msaidizi wa Polisi, GEORGE KYANDO aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo,ajali hiyo imetokea Jumapili june 19,katika barabara hiyo ya Tinde —Shinyanga eneo la kijiji cha Isela kata ya Ishinabulandi.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Gari lisilojulikana usajili na mmiliki wake likiendeshwa na dereva asiyejulikana jina lilimgonga mwendesha pikipiki huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 hadi 30 na kumsababishia kifo chake papo hapo.
Akizungumza Mwenyekiti wa mtaa wa Mbuyuni Bwana SEIF HEMED mahali alipokuwa akiishi marehemu ambaye ameeleza namna alivyopata taarifa hizo.
Taarifa nimezipokea tangu siku ya jana ambapo walikuja vijana kutoka stendi wakiwa wameambatana na Mwenyekiti wa waendesha bodaboda wakasema walikuwa wakimtafuta marehemu lakini walifikia kutoa taarifa polisi ndipo wakaambiwa mwili huo upo mochwali tumeukuta sehemu ndipo wakaenda kuuangalia na badae naye mke wa marehemu alienda kuangalia ule mwili akajirizisha kuwa ni kweli mume wake''. amesema Mwenyekiti Hemed
Kwa upande wake Mtoto wa Marehemu Stephen Juma ameeleza kuwa Baba yake aliaga nyumbani siku ya Jumamosi June 18, akielekea Nzega Mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya majukumu yake ya bodaboda.
Baba yangu alipigiwa simu ilikuwa siku ya Jumamos apeleke mzigo Nzega akaenda tu vizuri amefika kule akampa mzigo anayetakiwa kumpa sasa saa ya kurudi akampigia mama simu kwamba pikipiki imeharibika njiani alikuwa hana hela akatumiwa na rafiki yake akasema haya mi nitakuja mdogo mdogo toka huo muda hakupatikana tena yaani mpaka mwili umekuja kupatikana jana''. amesema Stephen Juma
Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Mbuyuni wameeleza walivyokuwa wakimfahamu marehemu huyo ambapo wamesema wameguswa sana na kifo hicho huku wakiliomba jeshi la polisi kuendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ili kuimarisha usalama wa raia na mali zake.
0 Comments