Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla amemtaka Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam Jumanne Shauri pamoja na menejimenti yake akiwemo Mkaguzi wa ndani na mweka hazina kutoa maelezo ndani ya siku 7 kutokana na upotevu wa fedha shill bill 10.137.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati alipokua katika kikao cha Baraza la madiwani wa jiji la Dar es Salaam wakati walipokua wakijadili taarifa ya mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ya mwaka wa fedha 2020/2021.
Aidha, amewataka mawakala wa ukusanyaji mapato na watumishi 19 wote waliotajwa katika taarifa hiyo ya kuhusika na upotevu wa shill bill 10.137 kurejesha pesa hizo ndani ya siku 60 kuanzia leo June 22, 2022.
"Nawataka mawakala wote na watumishi waliotajwa katika taarifa ya mkaguzibna Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ndani ya siku 60 kurejesha fedha zote munazodaiwa na endapo mutashindwa nitawakabidhi kwa takukuru"amesema RC Makalla.
Hatua hiyo, imekuja baada ya ukaguzi maalum wa ripoti ya CAG mwaka 2022/21 kuonyesha kiasi cha shill bill10 zilikusanywa lakini hazionekani kwenye mfumo ambapo wakala wamehusika na upotevu wa shill bill 4.5 na watumishi wa Halmashauri shill bill 5.4 na mpaka sasa hakuna aliyechukuliwa hatua.
Amesema kuwa, ameshangazwa na namna madiwani hao walivokua wanapitisha taarifa hiyo bila kuipa uzito wowote, ambapo ameeleza kuna majina ya watumishi na mawakala ambao wametajwa katika taarifa hiyo lakini hajaskia likitajwa hata jina moja.
"licha ya kuwa mmepata hati safi kwa miaka sita lakini taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG, lakini mapato hayaingii kwenye mfumo ndio maana kumetokea upotevu kama huu"amesema Makalla
Kwa upande wake, Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam Saady khimji amesema kuwa, anaimani kubwa na uongozi wa Mkurugenzi wa jiji hilo katika Utendaji wa kazi ispokuwa kuna baadhi ya wasaidizi wake ndio wanaomuangusha na kupelekea upotevu wa pesa nyingi ambazo hazionekani.
Aidha, amemtaka Mkurugenzi huyo baada ya kutoa maelezo yake kwa Mkuu wa Mkoa kuhakikisha wanafanya vikao kwa ajili ya kujadili namna gani suala hilo litaweza kumalizika, wahusika warejeshe pesa hizo bila kufikishwa takukuru.
Naye, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma amesema kuwa kitendo kilichofanyika leo ni cha aibu sana kwa Madiwani hao kujadili taarifa hewa ambayo haikuwafikia mezani mwao, huku akiwataka kujifunza kutokana na hilo.
0 Comments