Header Ads Widget

TUZO ZA ZIFF 2022 KUTOLEWA USIKU WA LEO TUZO 15 KUSHINDANIWA

 





TUZO zaidi ya 15, zinatarajiwa kutolewa usiku wa leo Juni 26, katika tamati ya tamasha la filamu za Nchi za Jahazi, [ZIFF], ambalo mwaka huu ni la msimu wa 25, kufanyika visiwani hapa.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa tamasha hilo, Prof. Martin Mhando, amesema zitatolewa tuzo hizo kwenye vipengele mbalimbali huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Zanzibar, Mhe. Simai Mohammed Said.


‘’Tumeweza kuonesha filamu 101, kutoka Mataifa tofauti zaidi ya 30.

Tuzo hizi zitaenda kwa miongoni mwa filamu hizo 101, kulingana na vigezo vya Majaji ‘JURY’ walivyozipitia.


…tuzo hizo ni pamoja na; kwa kipengele cha 

ZIFF GOLDEN DHOWS ni pamoja na; Tuzo bora ya filamu ya Ushirikishwaji [Best Feature Film],Tuzo bora ya filamu ya Afrika Mashariki [Best East African Films], Tuzo bora Documentari [Best Documentary],Tuzo bora fupi/Vikaragosi [Best Short  or Animation],



Pia tuzo ya Muigizaji bora wa Kike wa filamu Tanzania [Best Actress in Tanzania films], Muigizaji bora wa Kiume wa filamu wa Tanzania [Best Actor in Tanzania films], Muigizaji bora wa filamu wa kiume wa Afrika Mashariki [Best Actor in East African Films],  na Muigizaji bora wa Kike wa Afrika Mashariki [Best Actress in East African films].’’


Amezitaja tuzo zingine kuwa ni pamoja na tuzo za Sembene Ousmane chini ya GIZ.

Ambapo katika tuzo hizo za Sembene, washindi watatu watatunukiwa tuzo.


Aidha, tuzo za mwisho zitakuwa ni ‘Special Awards’ ambapo kutakuwa na tuzo za;

Tuzo ya Mwenyekiti [Chairperson’s Award or Bibi Kidude Awards.


Pia tuzo ya Maisha [Lifetime Achievement Award] na tuzo ya Wakfu ya Ermerson of Zanzibar Prize.


Aidha, mbali ya tuzo hizo, shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwemo burudani.



ZIFF imekuwa ikiwakuitanisha Waandaaji na waongoza filamu na wasanii mbalimbali katika kubadirishana mawazo na namna ya kusonga mbele katika masuala ya filamu ambapo pia filamu upata kuoneshwa katika kumbi tofauti pamoja na ndani ya jukwaa kubwa Ngome kongwe (Old fort).


Tamasha hilo lilizinduliwa rasmi usiku wa Juni 18, mwaka huu na Makamu wa Kwanza wa Rais  Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI