NA HADIJA OMARY _LINDI
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea ushirikiana na Taasisi zote za kidini zilizopo hapa Nchini katika kujenga mustakabali wa wananchi wake sasa na Baadae.
Majaliwa ameyasema hayo leo juni 26/2022 alipokuwa anazungumza na waumini wa madhehebu ya dini mbali mbali kwenye sherehe za ibada ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa asikofu wolfgang pisa kuwa askofu wa jimbo la Lindi baada ya kuteuliwa kwake na Mtakatifu fransisco siku chache zilizopita.
Majaliwa alisema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia suluhu Hassan inatambua na kuthamini kazi na majukumu makubwa ya viongozi wa dini mbali mbali ambayo ni pamoja na kuwaongoza watu ki roho kwa kuwa na mafundisho kutoa ushauri na kuwajenga kiimani .
Majaliwa aliongeza kuwa swala la kuwasaidia watu katika shida mbali mbali ususani wale wenye mahitaji kama mayatima, wajane na utoaji ushauri nasaha na malezi kwa vijana limekuwa ni kipaumbele kwa viongozi hao wa dini.
Alisema Serikali wakati wote imeendelea kushirikiana na dini zote katika Nyanja mbali mbali kwa lengo la kukuza ustawi wa wananchi kiuchumi na kijamii ili kuimarisha Maisha ya mtanzania mmoja mmoja kwa kuweka mazingira mazuri na fulsa mbali mbali za kuwekeza ili kufanya Maisha kuwa mazuri na yenye matumaini.
“Sina mashaka na kazi zinazoendelea kufanywa sasa na taasisi zote za kidini hasa katika utoaji wa huduma za jamii kwani mmejikita kuwekeza kwenye Elimu , afya , mmesaidia jamii yetu kwa kuwajengea visima vya maji , kuelimisha jamii kwenye sekta ya Kilimo na maeneo mengi ni matumaini yetu kwamba jukumu hilo litaendelea ”alisema
Majaliwa alisema kuwa ni ukweli usiopingika kwamba serikali pekeyake haitamudu kuwafikia watu wote kwa huduma katika maeneo hayo ambapo hata hivyo kutokana na jitihadi zinazofanywa na taasisi hizo za kidini Serikali imekuwa ikijivunia kwamba imeweza kufikisha huduma hizo mpaka kwenye vitongoji kwa msaada wao.
Pamoja na mambo mengine majaliwa alisema Serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto mbali mbali zinazozikabili Taasisi hizo ikiwa pamoja na ukubwa wa kodi zinazotozwa kwenye taasisi wanazotolea huduma kama vile hospitali na shule ili kuweza kujilidhisha juu ya shughuli zinazofanywa .
Alisema katika hili ni lazima taasisi hizo zikubali mkaguzi wa hesabu za Serikali azikague hesabu zao kwa kina ili kuweza kubaini ama kujiridhidha endapo Taasisi hizo zinajiendesha kibiashara ama zinatoa huduma ndipo tozo hizo zinaweza kupunguzwa baada ya kujilidhisha.
Awali Askofu Mkuu wa jimbo kuu Katoliki la Dodoma Mhashamu Beatus Kinyaiya alimtaka askofu huyo mpya wa Jimbo la Lindi mhasham Askofu asikofu wolfgang pisa ofm – Cap kuwafundisha waumini salaam pamoja na kufanya kazi ili waweze kumtumikia mung una kupata maendeleo wakiwa wanafanya kazi.
Pia alimtaka kushirikiana na mapadre wa jimbo hilo katika kuendeleza mema yote yaliyoachwa na mtangulizi wake askofu Bruno Ngonyani.
Akizungumza mara baada ya ibada hiyo ya kusimikwa kwake Askofu huyo Mpya wa Jimbo la Lindi wolfgang pisa aliahidu kudumisha upendo na amani kwa wananchi wote wa jimbo la Lindi.
Alisema pete aliyovalishwa leo wakati wa ibada ya kusimikwa kwake ni ishara tosha ya kwamba yeye kama Askofu amekubali kuwatumikia kondoo wa lindi na kwamba ameomba pamoja na kushukuru kwa mapokezi mazuri waliyoyaonyesha wananchi wa Mkoa wa Lindi ameomba ushiroikiano wao.
0 Comments