Header Ads Widget

JITIHADA ZATAKIWA KUONGEZWA ILI KUHAMASISHA KILIMO CHA KAHAWA

 



Na Gift Mongi_Moshi


Chama kikuu cha ushirika mkoani Kilimanjaro (KNCU)kimesema jitahada mbalimbali zinatakiwa kuongezwa ili kuhamasisha kilimo cha kahawa kama ambavyo mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi amekuwa akiishauri serikali.


Mwenyekiti wa chama hicho Jublethe Ndosi alisema kuwa kwa sasa zao la kahawa linalipa tofauti na miaka ya nyuma hivyo jitihada zinatakiwa kuwekwa kwa wakulima ili waweze kuongeza uzalishaji kwa wingi.


"Uzalishaji bado haujawa mzuri ikilinganishwa na miaka ya nyuma ila tunashukuru wapo wadau kama mbunge wa Moshi Vijijini Prof Nadakidemi mara kadhaa amekuwa akiishauri serikali kuona namna ya kuongeza nguvu ili kuzalisha kwa wingi zao hilo"alisema


Alisema kwa sasa kilo ya kahawa msimu uliopita bei ilikuwa ni shilingi 8500 bei ambayo ni ya juu zaidi ikilinganishwa na vyama vingine hivyo kuendelea kuimarika kwa soko hilo ni sawa na kwenda kuwahamasisha wakulima wazalishe kwa wingi zaidi.


Akichangia hoja ya bajeti bungeni wiki hii mbunge wa Moshi Viijini Prof Patrick Ndakidemi  alisema kuwa upo uwezekano wa zao la kahawa kutoa mchango mkubwa katika pato la taifa ni mkubwa japo kwa sasa limeshuka lakini bado ni zao la pili linaloingia serikali pato la kigeni lakini serikali ikiboresha zaidi zao hilo litaendelea kukua zaidi ya sasa.


" Zao la kahawa bado lina mchango mkubwa katika pato la taifa ikiwa ni pamoja na kuongeza au kuingizia taifa fedha za kigeni sasa naona ipo haja kwa serikali kuongeza  nguvu katika uzalishaji"alisema 


Alisema pia  serikali imesikiliza kilio cha wabunge na katika bajeti ya 2022-2023 imeongeza fedha katika bajeti ya kilimo itakayosaidia kupata mbegu bora na pembejeo pamoja na kuongeza mifereji mipya na kuboresha iliyopo kwa ajili ya kuendeshea kilimo cha umwagiliaji.


Mwenyekiti wa chama cha wenye viwanda na kilimo (TCCIA)wilaya ya Moshi Louis Mbuya alisema kama kutafanyika jitihada za maksudi katika ufufuaji wa kahawa ni dhahiri uchumi wa wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro utaenda kubadilika siku sio nyingi.


"Uhamasishaji usiachwe kwa wanasiasa pekee bali kila mmoja wetu na ninaamini kwamba kama tukilima kwa wingi na serikali ikatusaidia pembejeo basi uchumi wetu utaenda kubadilika siku sio nyingi"alisema


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI