Header Ads Widget

SERIKALI KUSHIRIKINA NA WAFANYABIASHARA, UBUNGO YAZINDUA KAMPENI YA ULIPAJI KODI KWA HIARI

 


Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam


Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Herry Jems amesema kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana na wafanyabiasha katika kuhakikisha maendeleo ya nchi ya Tanzania yanapatikana kupitia tozo, kodi na ushuru unaokusanywa kutoka kwa wafanyabiashara.


Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizindua rasmi kampeni ya kulipa kodi kwa hiari iliyoanzishwa mapema  Mei 5 mwaka huu yenye lengo la kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuweza kulipa kodi, tozo na ushuru kwa maendeleo ya Manispaa hiyo.


Amesema kuwa, dhamira ya Manispaa ya ubungo ni kuhakikisha pesa hizo zinakwenda kuchochea huduma na kukuza biashara na sio kwenda kuzifungia, hivyo amewataka wafanyabiashara waendelee kushirikiana na Serikali Ili kuweza kukuza miradi ya maendeleo.



Aidha amewataka maafisa biashara wa Manispaa hiyo kuwapa ushirikiano  wafanyabiashara pale wanapohitaji huduma, na sio kutokuwapokelea simu zao, huku akiwataka kuweka wazi milango muda wowote kwa ajili ya kuwahudimia.


"Kipindi cha kampeni mlikua nao karibu walipa ushirikiano wa kutosha, waliwaeleza kwa sababu za wao kutolipa kodi, hakukua na uwelewa wa kutosha, tuna tabia ya kufunga maduka kwa wafanyabiashara kutolipa kodi, tozo na ushuru, hivi ni vitu vinavyo zungumzika na tukifanya hivyo walipa kodi wataongezeka, tija itaonekana na biashara itakua"amesema Jems.



Kwa upande wake, Mwanasheria wa Manispaa ya ubungo Fortunata Shija ambae alikua anamwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, amesema kuwa, lengo la kampeni hiyo ilianza kwa lengo la kuwajengea uwelewa wafanyabiashara juu ya kuweza kulipa kodi, ushuru na tozo kwa wakati, ambapo kampeni hiyo imeweza kutoa matokeo chanya kwani wananchi wameweza kuelewa wajibu wao.


"Baada ya hii kampeni tumekubaliana itakua endelevu na tumeanza kutembelea maeneo manne ya Manispaa ya Ubungo ikiwemo Manzese na Sinza, tunazo Kata 14 katika Manispaa yetu tutahakikisha tunapita kila sehemu kuwaelimisha wananchi namna ya kulipa kodi, tozo na ushuru na faida zake katika kuleta maendeleo kwa Taifa"amesema Fortunata.



Naye, Mfanyabiashara wa Mbezi Louis Robert Minja amesema kupitia kampeni hiyo ameweza kulipa kodi na ushuru kwa urahisi zaidi kwani imewapa elimu juu ya umuhimu wa wao kuweza kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa la Tanzania.


"Kwa sasa tupo huru tumeupata sehemu ya kupeleka malalamiko yetu na tukasikilizwa zamani kulikua hakuna ushirikishwaji walikua wanakuja na kufunga maduka yetu hatukua na uwelewa ila kwa sasa hata mimi naweza kuwa Balozi"amesema Minja.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI