Header Ads Widget

TAASISI YA MIFUPA (MOI) WATAKIWA KUBORESHA HUDUMA KWA WATEJA

 


Na.WAF-DSM


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu Ameitaka Taasisi ya mifupa (MOI) kuboresha huduma kwa wateja ili kuweza kupunguza msongamano wa wagonjwa na kutoa huduma bora za Afya kwa wananchi


Ameyasema hayo leo katika ziara yake alipoitembelea Taasisi hiyo ili kuona hali ya utoaji wa huduma za Afya sambamba na kusikiliza kero za wananchi wanaofika hospitalini hapo.


Waziri Ummy amesema kuna baadhi ya madaktari wana tabia ya kuwarudisha wagonjwa nyumbani bila kupata huduma japokuwa wamekaa muda mrefu 


"Haiwezekani mtu anakuja zaidi ya mwaka na nusu hospitali anaambiwa arudi baada ya wiki mbili, kama ni mgonjwa amekuja kwa ajili ya upasuaji na wataalamu wameona hayupo tayari aambiwe mapema" Amesema Waziri Ummy



Pia Mhe. Ummy amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa MOI kufuatilia na kukomesha tabia ya baadhi ya madaktari kuwaandikia wagonjwa vipimo na kuwataka kwenda kufanya katika Hospitali binafsi japokuwa vipimo hivyo vinapatikana hapo


"Swala hili hatutalifumbia macho, Mtu anakuja akidhani atapata vipimo kwa bei nafuu lakini anaambiwa aende kwenye kituo cha nje hii haikubaliki ni lazima tuwapunguzie mzigo wananchi"Amesema Mhe. Ummy


Aidha, Waziri Ummy amesema Wizara ya Afya imejipanga kuimarisha huduma za Afya katika hospitali za rufaa za kanda ili kuweza kuzipunguzia mzigo hospitali za taifa.



"Tumeona wagonjwa wanatoka katika mikoa mbalimbali kama wizara ya afya ni lazima tukawekeze zaidi katika hospitali za kanda ili wagonjwa waweze kutibiwa kule walipo, "


Pia Mhe Ummy amewataka madaktari bingwa wa MOI kuwa na mpango wa kwenda mikoani mara kwa mara kwa ajili ya kutoa huduma ili kuwapunguzia wananchi usumbufu wa kusafiri hadi jijini Dar es Salaam.


Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa MOI Dkt.Respicious Boniface amesema Taasisi ya MOI inaendelea kujipanga na kukabiliana na msongamano wa wagonjwa kwa kupanga shift mbali mbali za kuona wagonjwa licha ya kukabiliwa na changamoto ya ufinyu wa majengo.




"kwa sasa hospitali ya MOI ina ona wagonjwa 500 mpaka 700 kwa siku na majengo yake yalijengwa mwaka 2003 yenye uwezo wa kuona wagonjwa 100 mpaka 150 kwa siku "



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI