Header Ads Widget

ROYA TOUR YATAMBULISHWA RASMI KWA WANANCHI MWANZA



Kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa huo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Maono ya kuitangaza nchi kwa kuamua kufanya filamu ya Royal Tour ambayo imeitangaza nchi kwa viwango vya kimataifa.


Amebainisha hayo kwa furaha kwenye viwanja vya Rock City Mall leo alasiri Juni 18, ,2023 viwanjani Rock City Mall wakati wa Utambulisho Rasmi wa Filamu ya Royal Tour kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza hafla iliyotanguliwa na Maandamano adhimu ya maelefu ya Wananchi.


"Tanzania imefunguliwa na Mwanza imefunguka hadi lengo la kupokea wageni kwenye kisiwa cha Saanane imeshavunja rekodi, wageni hao wote wamewapa wanamwanza fesha kwa kufanya nao biashara mbalimbali zikiwemo za mamalishe na wachuuzi." Mkuu wa Mkoa.



Ameongeza kuwa uwepo wa filamu ya Royal Tour wananchi wa Mwanza wamefarijika sana na sasahivi wananchi wa Mwanza ni wakati wa kutalii na kupumzika kwenye hifadhi na vivutio vilivyopo Mkoani hapo kwani baada ya kazi mtu anakwenda kisiwa cha Saanane anabarizi anawaona na Simba.


Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Mhe. Julias Peter amebainisha kuwa pamoja na kuitambulisha Nchi kupitia Filamu ya Royal Tour Mhe Rais anawapenda watanzania na wanaMwanza na amewaletea zaidi ya Shilingi Bilioni 600 kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Bilioni 383 kwenye miradi ya kimkakati. 


"Afisa Utalii Mwandamizi Mkuu wa Kanda, Bi Dainess Kunzugala amesema kuwa Sekta ya Utalii inachangia uchumi wa Nchi yetu kwa asilimia 17 na kwa asilimia 25 kwa fedha za kigeni na Mwanza ni kitovu cha utalii kwa kanda ya ziwa kwani ndipo sehemu ya katikati kufika hifadhi mbalimbali kama Serengeti na Burigi Chato.




"Sekta ya Utalii ni sekta muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu, tunamshukuru sana Mhe Rais kwa kuitangaza nchi kupitia filamu ya Royal Tour ambayo ameifanya yeye mwenyewe na kwa sasa tunapokea watalii wapatao milioni 1.5 na kupitia filamu hii tunatarajia wataongezeka hadi milioni 5." Amebainisha.


Kabla ya Uzinduzi rasmi wa filamu hiyo, wananchi wa Mkoa wa Mwanza walipata fursa ya kuangalia burudani kutoka kwa wasanii wa nyimbo na maigizo na ngoma za asili.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS