Header Ads Widget

MBUNGE MAKANIKA AKABIDHI GARI LA WAGONJWA KALINZI




Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MBUNGE wa jimbo la Kigoma Kaskazini Asa Makanika amekabidhi gari ya kubeba wagonjwa kwa kituo cha afya Kalinzi Halmashauri ya wilaya Kigoma ili isaidie kubeba wagonjwa wenye dharula kwenye kwenye vituo vya afya na hospitali kwa haraka.

 

Mbunge huyo amekabidhi gari hilo aina ya Toyota Hard Top kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kigoma,Exavery Ntambala katika katika hafla iliyofanyika kwenye Kijiji cha Kalinzi na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wananchi wa eneo hilo.

 

Akikabidhi gari mbunge alisema kuwa limetolewa kutokana na changamoto kubwa iliyokuwepo ambapo wagonjwa wenye dharula kutoka majumbani na zahanati Kwenda vituo vya afya na hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma halikuwepo na kulikuwa na matatizo Zaidi yaliyokuwa yakitokea kwa wagonjwa ambao walikosa usafiri kwa dharula zilizokuwa zikijitokeza.

 

Mbunge wa  jimbo la Kigoma kaskazini Asa Makanika (kulia) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kalinzi Halmashauri ya wilaya Kigoma muda mfupi kabla ya kukabidhi  gari la wagon jwa kwa kituo cha Afya Kalinzi Halmashauri ya wilaya Kigoma lililotolewa na serikali katika mpango wa serikali ya Raisi Samia Suluhu Hassan Kuboresha utoaji katika sekta ya afya.

(Picha na Fadhili Abdallah)

Akipokea gari hilo kwa niaba ya kituo cha afya Kalinzi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kigoma,Exavery Ntambala alisema kuwa ujio wa gari hilo utapunguza matatizo kwa wananchi wenye dharula hasa mama wajawazito na Watoto.

 

Ntambala alisema kuwa gari hilo ni miongoni ma mipango ya uboreshaji wa huduma za afya nchini ambazo zinasimamiwa na Raisi Samia Suluhu Hassan na kwamba kwa miaka hii mitatu ambayo mbunge huyo yupo madarakani vituo vitatu vya afya vimejengwa na kukamilika ikiwa ni juhudi kubwa ya mbunge huyo kuzifikisha hoja za mahitaji hayo kwa serikali.

Akizungumza katika makabidhiano Mwenyekiti wa CCM wilaya Kigoma Vijijini, Halmeshi Mayonga ameponga serikali ya Raisi Samia kwa kazi kubwa aliyofanya katika kuboresha sekta ya afya sambamba na kumpongeza mbunge Asa Makanika ambaye amefanya juhudi kubwa kuhakikisha miradi mbalimbali ya wananchi inaletwa kwenye jimbo lake.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI