Header Ads Widget

MRADI MIAKA MITANO WA UBORESHAJI WA ELIMU NCHINI WAZINDULIWA

Na Teddy Kilanga , MatukioDaimaAPP,Arusha

Katika kuhimarisha sekta ya elimu nchini Serikali imezindua mradi wa kuboresha upatikanaji wa fursa sawa katika utunzaji bora wa elimu ya awali na msingi Tanzania bara(Boost) unaogharimu takribani sh.tirioni 1.15 ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano

Akizungumza Juni 6,2022 jijini Arusha katika uzinduzi wa programu hiyo,Waziri wa elimu , Sayansi na Teknolojia,Prof.Adolfu Mkenda amesema mradi huo umefadhiliwa na benki ya dunia kwa lengo kuhimarisha nyanja mbalimbali katika sekta ya elimu kuanzia ngazi ya elimu ya awali.

"Mradi huu unatarajiwa kutoa matokeo muhimu na kuhimarisha mfumo wetu wa elimu katika ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa 12000 na vifaa vya shule vinavyohusika katika maeneo yenye uhitaji zaidi,"amesema Waziri Mkenda.

Pia amesema matokeo mengine ni pamoja na kuanzishwa kwa vituo vya walimu na kuendelezwa kwa ajili ya utoaji wa mafunzo kwa njia ya TEHAMA kupitia maktaba mtandao,shule za msingi 6000 kuwezeshwa kutekeleza programu za shule  msingi salama.

"Mradi huu utasaidia kuongezeka kwa uwiano wa uandikishwaji wa wanafunzi wa elimu ya awali kutoka asilimia 76.9 hadi 85 pamoja na kuongeza kiwango cha wanafunzi kubaki shuleni katika halmashauri zilizo katika kundi la robo ya chini kutoka asilimia 55.9 hadi 66.2,"amesema Prof.Mkenda.

Kamishna wa elimu Tanzania Dk.Lyabwene Mtahabwa alisema mradi huu unajenga watoto kuanzi ngazi ya shule ya awali hivyo serikali imeamua kutumia mbinu ya kurekebisha hali ya kukabiliana na ufisadi na kuweza kuwa mzalendo katika nchi yake.


Dkt.Mtahabwa amesema programu ya boost ni mpango wa lipa kulingana na matokeo katika elimu yaani (EPforR II) ikiwa maandalizi ya utekelezaji yameshakamilika kutokana na majadiliano mbalimbali kati ya serikali na Benki ya dunia katika uendeshaji wake.

"Programu hii ya boost imetokana na changamoto  zilizobainika katika uchambuzi wa taarifa za sekta ya elimu ya mwaka 2021 ambazo zinaathiri utoaji wa elimu bora kwenye ngazi ya elimu msingi,"amesema.

Amesema baadhi ya changamoto hizo ni kuwepo kwa msongamano wa wanafunzi madarasani kutokana na uhaba wa miundombinu wa madarasa,baadhi ya shule kutokuwa na mazingira rafiki ya ujifunzaji na ukosefu wa vifaa vya ufundishaji wa elimu ya awali.


Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Said Mtanda alisema anashukuru wizara ya elimu ,Tamisemi pamoja na World benki kwa kuleta mradi huo na wako tayari kuusimamia katika kuleta chachu ya maendeleo kwenye sekta ya elimu.

Mkurugenzi mkaazi wa benki ya dunia,Mara Warwick amesema mradi huu unaongeza nafasi ya watoto wengi kupata elimu ya awali na msingi pamoja na kuongeza ushindani wa uwajibikaji kwa walimu.

"Mradi huu utawanufaisha zaidi ya wanafunzi milioni 12 hivya naiomba serikali ya Tanzania kuondoa baadhi ya vikwazo vinavyozuia watoto kushindwa kupata elimu msingi,"amesema Warwick.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI