Na Amon Mtega,_Madaba
Mbunge wa Jimbo la Madaba Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Dr.Joseph Mhagama atoa jezi kwenye timu zaidi ya 50 zilizopo kwenye Vijiji vya Jimbo hilo kwa lengo la kuibua vipaji vya michezo na kuipata timu bora ya Halmashauri ya Madaba.
Akikabidhi jezi kwenye timu hizo Mbunge huyo amesema kuwa amefikia maamuzi hayo baada ya kubaini kuwa kuna vijana wengi wanavipaji vya michezo lakini hawaendelezwi jambo ambalo limekuwa likisababisha vipaji vingi kupotea.
Amesema kuwa vipaji hivyo vitaibuliwa kwenye maeneo yao watakapokuwa wanacheza na kuwa mwisho wa siku itapatikana timu bora ya Halmashauri ambayo itaenda kushindana na timu nyingine nje ya jimbo hilo.
Kwa upande wake mchezaji mkongwe wa zamani Fred Mbuna amesema kuwa baadhi Vijana wenye uwezo wa soka hawajitambui kuwa viungo vyao kama miguu inaweza kuwaingizia uchumi katika maisha yao.
Mbuna ambaye amechezea timu ya Yanga, Majimaji pia kuwa kepteni kwenye timu ya Taifa stars ndiye atakayefanya kazi ya kuiunda timu ya Halmashauri kwa kupata wachezaji wenye vipaji .
Amesema kuwa soka sasa hivi linalipa na ni ajira hivyo hakuna sababu ya mtu mwenye kipaji kushindwa kukiendeleza kwa manufaa ya maisha yake.
Katika kukabidhi jezi hizo na mipira nao Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS)shamba la Wino kupitia mhifadhi mkuu shamba la miti Wino Glory Kasmir nao pia wamechangia jezi zenye dhamani ya zaidi ya milioni mbili.
Hata hivyo kukabidhi kwa jezi hizo imeenda sambamba na kutambua vipaji vya wasanii wa nyimbo za kizazi kimpya ambapo msanii George Mgaya (Sparo)pamoja na ZDM kutoka Songea walionyesha vipaji vyao huku wakiwataka vijana wenzao wasikate tamaa.
0 Comments