Na Frederick Siwale - Matukio daima Makambako Njombe.
WANAMICHEZO wa Makambako Jogging club wamepigwa jeki ya vifaa vya kuvaa wakati wakifanya mazoezi ya kukimbia na viungo.
Akikabidhi vifaa hivyo tisheti 30 na viakisi mwanga (reflector) 30 Mfariji Malekela mkazi wa Jijini Dar es salaam na mzawa wa Makambako mkoani Njombe ,alisema baada ya kuona na kusikia kuwa Makambako kuna Jogging club imeanzishwa aliamua kusafiri ili kujiridhisha.
Malekela alisema aliwiwa kuwaunga mkono waanzilishi wa Makambako Jogging club baada ya kuona kila mmoja anavaa vazi lake ambalo halionyeshi kuwa ni la kimichezo.
" Nimeamua kutoa vifaa hivyo na ikibidi nitaendelea kufanya hivyo ili kuwapa motisha ya wanamichezo kujitokeza kwa wingi kushiriki Jogging hii" Alisema Malekela.
Malekela alipongeza Uongozi wa Makambako Jogging club kwa kuanzisha klabu hiyo ambayo itasaidia Watu kufanya mazoezi asili badala ya kufuta mazoezi yanayotumia vifaa vya kidgital.
Makambako Jogging club itakuwa ni chachu kwa Wana Makambako Vijana na Wazee kupenda kufanya mazoezi bila kutumia gharama .
Upande wake mmoja wa Viongozi wa Klabu hiyo Joseph Masekhoo "DJ Jozee " akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Makambako Jogging club Nassoro Chang'a alimshukuru Mdau Mfariji Malekela kwa kuonyesha moyo huo wa upendo kwa Wana Makambako Jogging club na kuomba wengine waige tabia ya kujitolea kwa faida na maslahi ya walio wengi.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Jimbo la Makambako Ally Mhagama ,alikabidhi viaksi mwanga 20 kwa Uongozi wa Makambako Jogging club kama zawadi kwa kuanzishwa kwake.
"Nitajisikia fahari iwapo vijana katika Halmashauri ya Mji Makambako watajitokeza kwa wingi kujiunga na mazoezi kupitia Kikundi hicho cha Makambako Jogging club.
Masekhoo alisema kwa kawaida kipindi kama hiki cha baridi watu wengi wanapenda kulala usingizi kwa kuwa hakuna sehemu ya kwenda na hivyo mazoezi yatasaidia.
"Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Makambako Jogging club nizidi kuwaomba wadau mbali mbali ziikiwepo taasisi za Umma na binafsi kuendelea kusaidia vifaa mbali mbali vya michezo ili kutengeneza jamii yenye kupenda michezo." Alisema Masekhoo.
Aidha alisema Klabu hiyo imeanzishwa kwa lengo la kuihamasisha jamii kupenda mazoezi na kwamba Mazoezi ni afya.
Ally Mhagama -Mwenyekiti Uvccm Jimbo la Makambako mwenye shati nyeupe akikabidhi vikoti 20 viakisi mwanga kwa Joseph Masekhoo wa Makambako Jogging club.
0 Comments