Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi akitazama ajali ya Costa iliyoua watu 20
WATU 20 wamefariki dunia na wengine 7 kujeruhiwa katika ajari iliyohusisha Lori aina ya scania na coster iliyotoka eneo la changarawe Mjini Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa alfajili ya jana .Mwandishi Francis Godwin MatukioDaimaAPP,Iringa
Ajali hiyo imehusisha gari aina ya Scania yenye namba za Usajiri T 736 AAE na Coaster yenye namba za usajiri T542 DQV
Wakizungumza na mwandishi wa Habari hizi eneo la tukio baadhi ya mashuhuda akiwemo John Kyando na Kefa Sanga walisema baada ya ajali ya Costa maiti zilizotolewa ni 7 na Majeruhi ndio walikuwa wengi wamelazwa chini kabla ya kugongwa na Lori jingine .
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mafinga Dr. Victor Msafiri alisema kuwa ajali hiyo iliyotokea imesababisha vifo vya watu 19 ambavyo vilitokea eneo la tukio na Majeruhi mmoja amefia wodini wakati akipatiwa matibabu
Alisema kuwa Majeruhi wanaendelea kupata matibabu na miilii ya marehemu baadhi imeshatambulika na wengine wanaendelea kutambuliwa .
Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi amethibitisha kutokea Kwa ajali hiyo na kuwa dereva wa Lori anashikiliwa na Polisi .
Kamanda Bukumbi alisema kuwa alisema kabla ya ajali ya Costa kwenye mteremko huo mkali kulikuwa na ajali ya Lori lililoanguka majira ya Saa 6 usiku wa kuamkia jana na kabla ya Costa hiyo kuligonga Lori Hilo na kupinduka na kupelekea vifo vya watu 7 papohapo na Majeruhi zaidi ya 16 .
Kamanda Bukumbi alisema vifo zaidi Katika ajali hiyo vilisababishwa na Lori ambalo liliferi breki na kuwagonga na kuwaua Majeruhi 12 waliokuwa wametolewa kwenye Costa na kulazwa kando ya barabara kuu ya Iringa -Mbeya wakisubiri kukimbizwa Hospitali .
Hivyo Kwa mujibu wa Kamanda Bukumbi ajali hiyo imehususha magari matatu yakiwemo Malori mawili na Costa mmoja maarufu Kwa jina la Hakuna Kulala iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda Mbeya .Wananchi wa Mufindi wakitazama ajali ya Costa na Lori iliyoua watu 20
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule akizungumza na wafiwa na ndugu wa Majeruhi eneo Hospitali ya wilaya ya Mufindi alisema Serikali itaendelea kuwasaidia Majeruhi hao na kuwa miili ambayo bado kutambuliwa itapelekwa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa Kwa kuhifadhiwa kutokana na chumba Cha kuhifadhi maiti Katika Hospitali ya Wilaya ya Mufindi kuwa kidogo
Ajali ya Majinja ilivyotokea Mei 13,2015
Hii ni ajali mbaya ya pili kutokea eneo hilo na kusababisha vifo vingi zaidi baada ya ajali la hiyo iliyohusisha Lori na basi la Majinja Kutokea eneo hilo Mei 13 mwaka 2015 na kusababisha vifo vya watu zaidi
0 Comments