Header Ads Widget

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AWACHANGIA WATOTO WA KIPAPA WA KANISA LA ROMANI JIMBO LA SONGEA


NA AMON MTEGA,MATUKIO DAIMAAPP

       SONGEA.

WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Jenista Mhagama amechangia fedha Sh,500,000 kwenye harambee ya uzinduzi wa Albamu ya nyimbo za kwaya ya watoto wa shirika la kipapa la Romani Katholiki Jimbo kuu la Songea.


 Akizungumza Cresensia Kapinga kwa niaba ya Waziri huyo kwenye harambee ya uzinduzi wa Albamu hiyo iliyofanyika ukumbi wa familia Takatifu Bombambili  mjini Songea amesema kuwa Waziri huyo amechangia fedha hiyo kutokana na kazi iliyofanywa na watoto wa shirika hilo.



Kapinga ambaye pia ni mwaandishi wa habari wa gazeti la Majira  amesema kuwa Waziri Mhagama ambaye alitakiwa kuwa mgeni rasmi kwenye tukio hilo ameamua kumtuma yeye kutokana na kubanwa na kazi za kitaifa kisha kuchangia fedha hizo.


"Waziri Jenista Mhagama amesema niwasalimie sana alitamani kuwa na ninyi siku ya leo lakini  kwa bahati mbaya amebanwa na kazi za kitaifa hivyo amesema pokeeni mchango huu na kuwa mambo mengine mtawasiliana zaidi"amesema Cresensia Kapinga.


Kwa upande wa watoto wa shirika la kipapa wakisoma risala lililosomwa na mwenyekiti wao Catherine Mpangala wamesema kuwa Albamu yao ina nyimbo nane na kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa usafiri .


Katika harambee hiyo ambayo imejumuisha watoto wa kipapa 200 na imehudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Naibu Askofu Ericki Mapunda imeweza kupatikana fedha sh.Milioni 4.2 zikiwemo na ahadi ambazo watu wameahidi.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI