Mwandishishi wetu
Mwanza.
Vijana wametakiwa kujiendeleza kielimu Ili waweze kupambana na soko la ajira na raia wa kigeni.
Kauli hiyo imetolewa na mkurugenzi Mtendaji wa Yuhoma Educational LTD , Yusuph Yahaya wakati akizungumza na waandishi Wa habari ofisini kwake.
Yahaya amesema serikali Kwa upande wake imeleta miradi mikubwa nchini lakini wataalamu wengi wanatoka kutoka nje ya Tanzania na watanzania wanabaki kufanyakazi zisizohitaji ujuzi.
Amesema elimu ndio njia pekee ambayo vijana wakiwemo wa wqandishi wa habari wanaweza kuitumia kupata ajira za uhakika na zenye maslahi makubwa.
Yuhoma Educational ltd ni Taasisi inayojihusisha na utoaji wa elimu nje ya nchi ambao watanzania wengi wameisha nufaika na taasisi hiyo.
Yuhoma Educational ltd ni miongoni mwa wadhamini wa Usiku wa Waandishi na Wadau Wa Habari Kanda ya Ziwa utakaofanyika tarehe 03/06/2022 katika ukumbi wa Rock City Mall.
0 Comments