Header Ads Widget

RAIS DKT. MWINYI MGENI RASMI UZINDUZI WA FILAMU YA ROYAL TOUR VISIWANI ZANZIBAR

  

      Rais Dkt Mwinyi 

Na Andrew Chale, Matukio  Daima APP Zanzibar. 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kesho Mei 7, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filamu yenye kutangaza Tanzania kwenye nyanja ya Utalii ya Royal Tour,uzinduzi utakaofanyika katika hoteli ya Zanzibar Golden Tulip Airport Hotel.


Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uzinduzi wa filamu ya Royal Tour, Dkt. Hassan Abbas akizungumza mapema leo Mei 6,2022 mjini Unguja, Zanzibar kuhusu maandalizi ya Uzinduzi huo visiwani hapa. (PICHA na Andrew Chale,  Matukio Daima App-Zanzibar)

Akizungumzia maandalizi ya uzinduzi huo leo Ijumaa Mei 6, 2022 Mwenyekiti wa kamati ya Taifa ya uzinduzi wa filamu hiyo, Dk Hassan Abbas amesema tayari maandalizi yamekamilika.


Dk Abbas amesema filamu hiyo inazinduliwa baada ya uzinduzi wa awali nchini Marekani, na kisha Arusha mwezi Aprili na sasa mwezi huu wa Mei wanaizindua Zanzibar kisha itaenda kumalizia uzinduzi wa mwisho Dar es Salaam ambapo siku hiyo filamu itarushwa yote moja kwa moja na kusambazwa katika media za ndani.


"Mei 7, 2022 hapa katika hoteli ya Golden Tulip Airport,  tunatarajia kuwa na mgeni rasmi Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye ataizindua rasmi.


Kutakuwa na wadau maalum wataishuhudia lakini pia siku inayofuata yaani Mei 8, itazinduliwa katika Jiji la Dar es Salaam na wa Tanzania wote wataishuhudia kupitia kwenye vyombo mbalimbali vya ndani vya habari." Alieleza Dk. Abbas.


Dk Abbas ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema filamu hiyo licha kuzinduliwa nchini pia tayari imewekwa kwenye mtandao wa Amazon wenye watu zaidi milioni 150.


Amesema pia filamu hiyo tayari imeanza kutazamwa na runinga 350 za majimbo nchini Marekani ambapo watu zaidi ya million 130 wanatarajia kuona.


Amesema serikali inatarajia watu bilioni moja kuiona filamu hiyo ndani ya muda mfupi na hivyo kuvutia mamilioni ya watalii duniani.


Aidha, alibainisha kuwa, filamu hiyo inakuwa ni ya kipekee kwani ndo iliyoweza kuhusisha viongozi wakuu wa nchi zaidi wawili.


"Ndani ya filamu ya Royal Tour,  kuna Marais Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na pia kuna Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi, utaona hapo umuhimu wake,


Ndani kuna vitu mbalimbali vimepangilia kwa mpangilio wa hali ya juu, tunaenda kuiweka Tanzania kwenye ramani ya kimataifa kupitia Utalii


Lakini pia Rais Mhe. Samia amepata kukutana na matajiri wakubwa watano ambao wameonesha kuja Tanzania kuwekeza kwenye utalii akiwemo anayemiliki meli kubwa za kifahari ambapo wataleta wageni Tanzania na meli hizo zitatia nanga kwenye maeneo yetu haya" alisema Dkt. Abbas.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI