Header Ads Widget

WANANCHI NJOMBE WAHIMIZWA KUTUMIA VIFAA VYA KUZIMIA MOTO .

 



Na Frederick Siwale -Matukio daima tv Njombe.


WANANCHI Wamehimizwa kufahamu matumizi ya vifaa za kuzimia moto pindi unapotokea ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi za tukio la moto na kwa wakati.                                 



Wito huo umetolewa mei 6 mwaka 2022 na Kaimu kamanda wa Jeshi la kikosi cha zimamoto Mkoani Njombe Mkaguzi Joel Mwakanyasa wakati wa ukaguzi na elimu ya matumizi sahihi ya vifaa vya kuzimia moto akiwa stendi ya Mabasi Makambako.       


Bw.Mwakanyasa alisema ukaguzi na elimu hii inatolewa kwa Wananchi ikiwa ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya wiki ya Zimamoto inayotarajiwa kufanyanyika mei 8 mwaka huu 2020 kimkoa.                              



Alisema kumekuwa na dhana isiyokuwa na tija kwa wahudumu wa magari na hasa mabasi kubeba mtungi wa kuzimia moto ambao hauna poda au gesi ama ukiwa haufanyi kazi zaidi ya kuwa wa mapambo kwa abiria kuaminishwa kuwa kuna kifaa cha kuzimia moto.                      


" Kifaa kibovu ndani ya gari  ni urembo usio na tija kwa kwa dereva na hata kwa abiria bali ni kuongeza uzito ndani ya gari ,hakikisheni mnakuwa na kifaa cha kuzimia moto na pia muwe mnafahamu matumizi yake" Alisema Mwakanyasa.          



Hivi kuna sababu gani ya kubeba mtungi wa kuzimia moto ambao hauna poda na haujawahi kukaguliwa na upo ndani ya gari zaidi ya miaka mitatu haujawahi kuguswa wala kukaguliwa au unawekwa karibu na mahali ilipo injini? Bw.Mwakanyasa alihoji.                                              


Pia alitoa elimu kwa Abiria kuhusu matumizi ya vifaa vya kuzimia moto na matumizi sahihi ya majiko yanayotumia mitungi ya gesi kwa kuwataka kufanya mabadiliko ya mipira ya kupitisha gesi kutona kwenye mtungi kupeleka kwenye niko kila baada ya muda wa mwaka mmoja.                 


Alisema matukio mengi ya majanga ya mitungi ya gesi kulipuka mara nyingi inatokana na uchakavu wa miundo mbinu ya kupitisha gesi na hasa mipira na hivyo kupelekea uvujaji hovyo wa gesi .    


Pamoja na elimu hiyo Bw.Mwakanyasa aliwataka Wananchi pindi tukio la moto linapotokea wahakikishe wanatoa taarifa sashihi na kwa wakati ili kuepuka lawama za kuchelewa kufika eneo la tukio ikiwa ni pamoja na anwani kamili au maelekezo  kuhusu tukio la moto lilipotokea.                                


Kazi hiyo ya elimu imefanywa kwa ushirikiano wa Jeshi la kikosi cha zimamoto na uokoaji Makambako, Kikosi cha Usalama barabarani Wilaya ya Kipolisi Makambako na Chama cha kutetea abiria (CHAKUA) Tanzania ,Kanda ya nyanda za juu kusini.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI