Header Ads Widget

NMB KUIPIGA JEKI HALMASHAURI YA MASASI UTATUZI CHANGAMOTO YA MADAWATI

 


NA HADIJA OMARY _MTWARA.


Hatua ya Bank ya NMB ya kutoa msaada wa madawati 150 yenye thamani ya shilingi milioni 15 katika shule za Msingi Ndanda, chipite na Njenga halmashauri ya Masasi Mkoani Mtwara kumetajwa kusaidia upungufu wa Madawati katika Shule hizo.


Zoezi la kukabidhi madawati hayo lilifanyika  jana mai 19 kwa nyakati tofauti katika viwanja vya shule ya msingi Ndanda na Chipite wilayani masasi Mkoani Mtwara mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo BI.Claudia Peter.


Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Meneja wa Bank ya NMB Kanda ya Kusini Bi. Janeth Shango alisema kuwa Changamoto za Sekta ya Elimu kwa Kank ya NMB  jambo la kipaumbele ,kutokana na ukweli kwamba Elimu ndio ufunguo wa Maendeleo kwa Taifa lolote.




Alisema pamoja na  kutambua jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika kutatua changamoto mbali mbali katika Sekta ya elimu wao kama wadau pia wanao wajibu wa kuunga mkono jitihada hizo.



Hata hivyo Shango alieleza kuwa madawati hayo waliyoyakabidhi ni moja ya ushiriki wao katika maendeleo ya jamii na  wao kama Bank wanao wajibu wa kuhakikisha jamii inayowazunguka inanufaika kutokana na faida wanayoipata.



Akizungumza mara baada ya kupokea madawati hayo Mkuu wa Wilaya ya Masasi , Claudia Peter licha ya kuishukuru Bank ya NMB kwa msaada wa madawati waliyoyatoa kwa shule hizo na namna wanavyounga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha mazingiza ya kufundishia na kujifunzia hasa katika Wilaya hiyo pia aliwataka wanafunzi kuyatunza madawati hayo yaweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu.



Kwa upande wake Mwalimu wa shule ya msingi Ndanda Magnus Mnonjela alisema kuwa Shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 677 ina uhitaji wa madawati  230 ambapo yaliyopo kwa sasa 166 hali hiyo inawafanya wanafunzi kulazimika kukaa dawati moja Watoto wanne hadi watano badala ya watatu hali hiyo inawafanya kuto kuwa watulivu na wasikivu wanapokuwa darasani.




“Niwashukuru sana Bank ya NMB kwani  baada ya kupokea msaada huo utawasaidia kupunguza changamoto ya madawati kwakuwa sasa baada ya wanafunzi kukaa wanne wanne sasa watakaa watatu watatu hii itawafanya wanafunzi kukaa kwa nafasi na kuelewa vizuri  mwalimu anachokifundisha Darasani hata hivyo kwa sasa tutakuwa na upungufu wa madawati 19 ambayo yangeweza kutosheleza kwa Watoto wote ”


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI