Header Ads Widget

TAASISI YA WANAWAKE 100,000 YAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUONGEZA ASILIMIA 23.3

 



Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Taasisi isiyokua ya Kiserikali ya Wanawake Laki moja (100,000) imempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa nyongeza ya kima cha chini cha msharaha cha asilimia 23.3.


Aidha, pia imempongeza kwa jitihada za kuitangaza Tanzania pamoja na vivutio vyake vya Utalii kupitia filamu ya Royal Tuor iliyozinduliwa hivi karibuni nchini Marekani pamoja na kukabiliana na ongezeko la bei ya mafuta duniani.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Vicky Kamata amesema Rais Samia ameonyesha ujasiri wa kipekee, ubunifu na uthubutu katika kukabiliana na changamoto zinazotokea nchini na duniani kwa ujumla.


Aidha, amesema Taasisi hiyo ina lengo la kuzunguka nchi nzima Ili kuwainganisha wanawake wote wenye uhitaji na kuwatoa sehemu moja kwenda nyengine kiuwezo, huku akiwataka wajiunge na Taasisi hiyo Ili kuondokana na utegemezi kwa wanaume.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Haki wa Taasisi hiyo, Josephine Matiro amesema Ongezeko hilo la mshahara ni kubwa kutokea nchini kwa  kipindi kirefu, hivyo imepelekea kuondoa vilio vya muda mrefu kwa wafanyakazi.


"Kupandishwa kwa mishahara kwa wafanyakazi wa Umma sio jambo jema kwa umma pekee bali kwa Taifa zima, kwani fedha hizo zitaweza kuingia kwenye mzunguko katika maisha ya kawaida ambapo wananchi wengi wataweza kufaidika na ongezeko hilo"amesema Josephine.


Hata hivyo, amesema utafiti wa wachumi huonyesha kuwa ongezeko la mishahara huleta chachi kwenye jamii yote na kuongeza pato la Taifa na kukuza uchumi kwa ujumla.


Naye, Mkurugenzi wa Miradi wa Taasisi hiyo na Balozi wa Utalii, Nangasu Warema amesema Filamu ya Royal Tuor itasaidia kutangaza fursa za Utalii na uwekezaji hapa nchini ambazo hazijawahi kutokea tangu chini ipate huru takriban miaka 60.


"Sote tunafahamu nchi jirani kutumia mabilion ya pesa kutangaza Utalii wao duniani, huku Tanzania ikiachwa nyuma hadi kupelekea baadhi ya watu huko nje kulaghaiwa kuwa mlima Kilimanjaro na Mbuga ya Serengeti ziko nchi jirani na sio Tanzania"amesema Warema.


Hata hivyo, amesisitiza kuwa Royal Tuor sio movie kama zile zinazotengenezwa Hollywood au Bollywood au Nollywood ama Bongo movie bali ni makala maalum inayotoa fursa za kipekee na mahususi ya kuitangaza Tanzania ulimwenguni kama kitovu Cha Utalii na uwekezaji duniani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI