Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Makame Mbarawa ameruhusu daraja la Chang'ombe kutumika rasmi kuanzia leo Ili kupunguza msongano wa magari yanayotoka Gongolamboto kwenda mjini ambayo imekua ni kero kubwa kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati alipokua katika daraja hilo amesema wananchi wamekua wakipata shida kutokana na foleni kubwa wakati wa asubuhi na jioni katika barabara ya Nyerere kutokana na ujenzi wa daraja hilo.
"Mimi sina mamlaka ya kufungua daraja hili, mwenye uwezo huo ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ila mimi nimekuja kuruhusu itumike Ili kuepusha msongamano wa magari"amesema Waziri Mbarawa.
Aidha, amewataka madereva wampatie ushirikiano mkandarasi kwa kufata alama ambazo watawekewa kwasababu Barabara bado ipo kwenye ujenzi wamefungua ili kuwasaidia kupunguza msongamano waweze kufika haraka zaidi katika maeneo yao ya kazi na wakati wa kurudi nyumbani.
Hata hivyo, amemtaka mkandarasi huyo Hadi kufikia mwezi wa 10 mwaka huu upande uliobakia wa daraja hilo uwe umeshakamilika Ili ziweze kutumika barabara zote na sio kama ambavyo inatumika sasa hivi.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu TANROAD Mhandisi Deodatus Matimbila amesema barabara hiyo inaviwango vya barabara kuu kama nyingine na inauwezo wa kubeba magari yenye tani 56 ambapo ujenzi huo wa BRT Two utapunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
"Barabara hii tulioifungua itakuwa inapita magari kutoka Gongo la Mboto kwenda mjini kwa asubuhi na jioni yatapita njia mistari miwili mmoja kwenda mjini na mwengine Gongo la Mboto "amesema Matimbila.
Naye, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam Abdi Isango amesema wanategemea kupunguza foleni na ajali ambazo zinatokea kutokana na msongamano uliokuepo awali huku akiwataka madereva kufata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali .
0 Comments