NA HADIJA OMARY
LINDI.....Katika kuboresha taaluma kwa watoto wa kike Mkoani Lindi , Serikali imetoa kiasi cha Shilingi milioni 4 kwa ajili ya ujenzi wa shule maalumu ya Wasichana inayojengwa katika kata ya kilangala manispaa ya Lindi Mkoani humo
Katibu wa Itikadi na uenezi chama cha Mapinduzi CCM Shaka Hamidu Shaka leo mei 30 ameshiriki katika ujenzi wa shule hiyo katika kuunga jitihada za Serikali
Akizungumza na wananchi Shaka aliwataka wasimamizi wa Mradi huo kukamilisha kwa wakati ili uweze kuleta tija kwa jamii
Alisema lengo la Rais Samia kutoa fedha kwa ajili ya kujenga majengo ya kisasa na kuweka vifaa vinavyowavutia watoto kisaikolojia kupenda shule ni katika kuweka usawa kwa jinsia zote
Alisema kuwa ujenzi wa Shule hiyo ya wasichana ni miongoni mwa shule 10 zinazotarajiwa kujengwa hapa Nchini ambazo zimetengewa kiasi cha shilingi milioni tatu kila shule mmoja
Hata hivyo pamoja na mambo mengine Shaka aliwataka wazazi na walenzi Mkoani Huko kuhakikisha wanaungana kwa pamoja kupiga vita mambo yote yanayomdhalilisha Mtoto wa kike
Awali akitoa taarifa ya Mradi huo Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Lindi, Rehema Nahale alisema Ujenzi wa shule hiyo kubwa kuliko zote zilizopo Mkoa wa Lindi na Mtwara umeanza kutekelezwa mai 5 mwaka huu .
Shule hiyo ya wasichana wenye vipaji na ufaulu wa kipekee ni ya kidato cha kwanza na cha sita ambapo mara tu itakapokamilika itakuwa na uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 800.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi Zainab Telack alisema Mkkoa huo wa Lindi kwa miaka mitatu mfululizo umekuwa ukiongoza katika Matokeo ya kidato cha sita , huku akieleza kwamba ni mwaka jana tu imekuwa nafasi ya pili kitaifa hii ni baada ya shule moja kutoa watoto wanne kupata daraja la tatu.
Alisema Kutokana na usimamizi mkubwa unaofanywa na maafisa Elimu na wakuu wa Shule wa ufundishaji na usimamiaji wa Taaluma ndani ya Mkoa huo wa Lindi wanafunzi wengi watafaulu kwenda kidato cha tano na wengi wao watabaki katika mkoa huo
Mwisho
0 Comments