Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Imeelezwa kuwa kati wananchi milioni 5.2 wanaoishi Mkoa wa Dar es Salaam kati ya hao ni mil 1.9 tu ndio wenye ajira ikiwemo kujiajiri wenyewe kama vile bodaboda na wengine wameajiriwa, huku jitihada za makusudi zikihitajika kuchukuliwa Ili kukabiliana na changamoto za ukosefu wa ajira.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Kaimu Meneja wa Takwimu za za Ajira na bei James Mbongo wakati akitoa usambazaji wa matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2020/21 katika Mkutano uliowakutanisha viongozi wa Kata na Mitaa wa jiji la Dar es Salaam.
Aidha, amesema kuwa utafiti huo umefanywa na Osifi ya Takwimu NBS kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Ofisi ya Takwimu Zanzibar.
Aidha, amesema utafifi huo umehusisha maeneo ya mijini na vijijini ambapo kuna changamoto kubwa ya ajira inayolikumba Jiji la Dar es Salaam ikilinganishwa na mikoa mengine ambapo asilimia 29 ya Wanawake hawana ajira huku wanaume wakiwa ni asilimia 12.
Hata hivyo, amesema kuwa, katika utafiti huo unaonesha bado kuna tatizo la ajira katika Jiji la Dar es Salaam ikilinganishwa na maeneo mengine na kuwataka watendaji wa kata kwenda kutatua changamoto hiyo kwa kuibua miradi mbalimbali.
Aidha, amesema katika tafiti hiyo imeonesha katika Sekta isiyorasmi kuna changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo kukopesheka na kupelekea kukosa maendeleo ya haraka huku asilimia 69 ya wanawake katika Jiji hilo wakiwa hawana kazi.
Akizungumzia suala la muda amesema kuwa kati ya masala 24 ya kazi wananchi hutumia masaa 3 tu kwa ajili ya shughuli za kiuchumi huku wanawake hutumia masaa 2 tu na wanaume hutumia masaa 4, huku wakitumia msaa 15 kwa ajili ya kupumzika.
Kwa upande wake, Godwin Mpelumbe ambaye ni Mtafiti Mkuu kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, amesema matokeo ya utafiti huo yana umuhimu kwa wizara kuyafanyia kazi maeneo yaliotajwa huku akiitaka jamii kuzidisha muda wa kufanya kazi ili kuweza kuongeza idadi ya ajira.
"Lazima watu wafanye kazi Ili uzalishaji ufanyike na waendelee kufanya kazi zenye tija kwani jiji la Dar es Salaam ndio limeonesha kuwa na idadi kubwa ya watu ambao hawana kazi"amesema Mpelumbe.
0 Comments