Header Ads Widget

KATA ZA URU SHIMBWE, KIBOSHO KATI NA MABOGINI ZAINGIZWA KATIKA MRADI WA TANZANIA YA KIDIGITALI.

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.



WANANCHI wa kata za Uru shimbwe, Kibosho kati na Mabogini katika jimbo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro wanatarajia kuondokana na adha ya usumbufu wa upatikanaji wa mtandao wa simu za mkononi baada ya serikali kuziingiza katika mradi wa Tanzania ya Kidigitali.

Neema hiyo imekuja baada ya Mbunge wa jimbo hilo, Profesa Patrick Ndakidemi kuhoji Bungeni serikali inampango gani kuboresha mawasiliano ya simu katika kata hizo tatu.



Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari, Mhandisi Kundo Mathew alisema kuwa, kata hizo zimeingizwa katika mradi wa Tanzania ya Kidigitali.


Aidha Naibu Waziri huyo alitumia pia nafasi hiyo kumpongeza Mbunge Ndakidemi kwa kazi kubwa anayoifanya kwa wananchi wake wa jimbo la Moshi vijijini.


Kwa upande wao wananchi wa maeneo hayo wamepokea kwa furaha huku wakidai kuwa wamekuwa wakipata mawasiliano kwa shida hivyo kuboreshwa kwa mawasiliano katika maeneo yao itakuwa fahari kubwa kwako.


Aidha walitumia pia nafasi hiyo kuipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hasani kwa jinsi ambavyo amekuwa akipambana kuhakikisha matatizo yanayowakabili wananchi yanapatiwa ufumbuzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI