Header Ads Widget

WAZIRI NAPE ASIFU ZOEZI LA UWEKAJI WA ANWANI ZA MAKAZI

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema kuwa kutokana na baadhi ya mikoa kutofanya vizuri katika zoezi linaloendelea la uwekaji wa anwani za makazi na posti kodi ,Wizara yake itafanya ziara ya kikazi mikoa yote nchini ili kubaini sababu zinazokwamisha ukamilishaji wa zoezi hilo .


pia amewataka wananchi kuhamasika juu ya umuhimu wa zoezi hilo .


Hayo ameyasema leo Aprili 11 jijini Dodoma wakati akijiandaa kuelekea Mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Arusha kwa ajili ya kuanza ziara hiyo ili kuhakikisha kila mkoa wananchi wanahamasika na kujua umuhimu wa Mfumo wa Anwani za makazi na post kodi .


Pia ameongeza kuwa mpaka sasa ni asilimia 69% tu ya maeneo yote nchini ndio zoezi hili limekamilika huku akisema kuwa Mkoa wa Lindi mpaka sasa ndio umefanya vizuri katika zoezi hilo huku Mkoa wa Dar es Salaam mpaka sasa haujafanya vizuri.


"Mpaka sasa mkoa wa Lindi unafanya vizuri katika zoezi hili ila kuna mikoa ikiwemo Dar es Salaam hawafanyi vizuri ninachowaomba mjitahidi kwa sababu mwezi ujao tarehe 25 ndio mwisho wa hili zoezi hivyo kila mmoja wetu ahakikishe amekamilika" Amesema Waziri Nape


Pia amewataka wamanchi kutambua kuwa jambo hilo la Anwani ya Makazi na Posti kodi ni la kwao hivyo kila mmoja aone aibu kukaa bila kuwa na anuani za makazi.


"Kila mmoja aone aibu kwa nini mpaka sasa hana anuani ya makazi hili jambo ni la kwetu sote ni faida ya kila mmoja litakusaidia kupata huduma bila kuchelewa naomba muone Aibu juu ya hili "Ameongeza Nape


Nape amemaliza kwa kusema kuwa Ziara hiyo wanategemea kupita mikoa mitatu hadi minne kwa siku ili kuendana na muda huu ambao umebaki mchache na kufanya havyo ana imani kuwa kila mwananchi atapata hamasi ya kutosha kuhakikisha anaingia kwenye mfumo huu wa anuani za makazi.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI