Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema suala zima la Elimu ni uwekezaji wa vizazi kwa vizazi na ukiwekeza katika elimu utakuwa umewekeza kwenye maendeleo ya Taifa kwa kizazi kimoja hadi kingine.
Akiongea leo jijini hapa wakati alipokuwa akifungua mkutano wa 30 wa Baraza la Wafanyakazi profesa Mkenda amesema uwekezaji mzuri katika elimu ni ule unahakikisha ubora wa Elimu ya sasa na vizazi vijavyo ambapo makosa yakitokea Basi makosa hayo yataendelea kuwa yale yale
"Katika nchi zote duniani ukiangalia vizuri tofauti yake Kubwa hipo katika uwezo wa kielimu hasa katika eneo la uwezo kielimu Sayansi na Teknolojia," amesema Prof Mkenda .
Amesema nchi zimekuwa zikipishana kwa mapato na kigezo kikubwa sio Rasilimali dhahabu Mafuta Wala madini kwani ziko nchi hazina Mafuta hazina Rasilimali lakini wamewekeza katika elimu kwa kuwekeza katika Sayansi na Teknolojia na wamefika mbali.
"Kwahiyo miradi hii iliyokuwa kwenye wizara yetu ya elimu tuingalie vizuri ili ije kutusaidie huku Prof Mkenda akiendelee kusisitiza Mfumo wa Elimu kufanyiwa maboresho ili kuleta maegeuzi kwa taifa na kuhakikisha vijana wanapomaliza shule wawe na uwezo wa kujiajiri au kuajiriwa.
Pia amezungumzia ubora wa elimu nchini kuwa unapaswa kupitiwa upya ili kumuandaa kijana kuwa mtaalamu huku akisema kuwa elimu haijakamilika ndio maana kuna baadhi ya vijana wanamalizi hadi vyuo vikuu lakini bado hawajakidhi katika taaluma waliosomea.
"Tunahitaji kuandaa Mtaala uliokamilika,embu tujiulize sote hapa kwa nini wataalamu wetu sio wazuri?,kwa sababu elimu yetu haijakamilika haimuandai kijana katika viwango vinavyotakiwa ndio maana nawaambia kuna haja ya kupitia upya Sera na mfumo wa elimu yetu,"Amesema Prof.Mkenda na kuongeza
"Tuna wajibu wa kutoa wataalamu wenye ubora na sio wataalamu wengi wasio na ubora niwaambie tu ni vigumu sana Watanzania kufaidika na matunda ya wataalamu wetu kwa sababu ya mfumo wa elimu yetu,"
Pamoja na hayo Prof.Mkenda amesema kuwa ubora wa elimu unakwenda sambamba na miundombinu bora na salama ya kujifunzia hivyo amewataka watumishi wa wizara hiyo kuhakikisha wanasimamia miradi inayoendelea ikamilike kwa wakati kwa sababu elimu ndio urithi wa vizazi vyote.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo Ambaye pia ni katibu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Eliamani Sedoyeka amesema kuwa baraza hilo lipo tayari katika kuhakikisha taratibu za Wafanyakazi na taratibu za uandaaji wa rasimu ya bajeti ya mwaka 2022/2023 ya wizara hiyo unaendelea kujikita katika kuwekeza kwenye maboresho ya elimu lengo likiwa ni kuwatengeneza wataalamu wenye ubora kwa ajili ya kuwasaidia watanzaina.
Naye Katibu wa CWT Deus G. Seif amesema kuwa bila kuwa na walimu wenye ubora katika Shule zetu tutaendelea kuzalisha watalaamu wasio na vigezo hivyo ni vyema kuhakikisha wanaotoa elimu kuwa na vigezo vya kutosha ili kusaidia hii taaluma inayotegemewa na taifa.
"Nataka niwahakikishie mwalimu akikosea gharama yake ni kubwa sana kuliko kosa kufanywa na daktari au Mhandisi kwa sababu unaweza kulirekebisha lakini kosa la mwalimu ni hatari sana,"Amesema Deus G.Seif
Mkutano wa 30 wa Baraza la Wafanyakazi la kujadili na kupitisha rasimu ya bajeti ya wizari hiyo ya mwaka wa 2022/2023 kabla ya kupelekwa bungeni inakwenda na kaulimbiu isemayo "Sensa ya watu na makazi ni Msingi ni kichocheo cha sera Bora na Mipango Endelevu ya elimu,Sayansi na Teknolojia, Tushiriki kikamilifu.
0 Comments