Header Ads Widget

WAZIRI NDALICHAKO ATOA MAAGIZO KWA WAAJIRI.



NA HAMIDA RAMADHAN,  DODOMA. 


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Ajira,Vijana na watu wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako amewaagiza waajiri wote nchini kuhakikisha vikao vyote vya baraza la wafanyakazi yanafanyika kwa mujibu wa sheria.


Profedsa Joyce ameyasema hayo jijini hapa wakati akifungua Mkutano wa Baraza Kuu la Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (TUCTA).


Amesema mabaraza yanapoisha muda wake wa kufanyika kunakuwa na kuchelewa kuyaunda upya.


“Vyama vya wafanyakazi vimeonyesha kufurahishwa na hatua ambazo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akizichukua kushughulikia masuala ambayo yanahusu wafanyakazi kuhusiana na mabaraza ya wafanyakazi ni takwa kisheria nachukua fursa hii kuwaagiza waajili wote kuhakikisha mabaraa ya wafanyakazi yanafanyika kwa wakati kwa mujibu wa sheria,”alisema


Amesema waajli wanatakiwa kutambua kuwa mabaraza ya wafanyakazini daraja kati ya waajili na waajiliwa ambalo lengo ni kufikisha masuala yanayohusu wafanyakazi na maslahi binafsi.


Kuhusu watumishi kuwekwa ndani kwa makosa yasiyokuwa ya kijinai waziri Ndalichako alisema serikali imeshatoa miongozo kwa wakuu wa Mikoa na Wilaya wasiweke watumishi ndani kwa makosa ambayo siyo ya jinai.


“Nachukua fursa hii kuwakumbusha wakuu wa mikoa na wilaya kutekeleza maelekezo ya serikali kwasababu wakati maelezo yanatolewa nilipewa nakala inayotoa maelekezo kwa wateule hao kuacha kuwaweka ndani watumishi kwenye masuala ambayo sio ya kijinai,”alieleza


Ameongeza kuwa “Serikali inataka kuona kuwa watumishi wanafanya kazi kwa kuzingatia mujibu wa sheria na pale wanapokosewa wanaadhibiwa kwa mujibu wa sheria zilizowekwa za kushughulikia masuala ya utovu wa nidhamu mahali pa kazi,


Kwa upande wake Rais wa TUCTA Tumain Nyamhokya alisema kikao hicho ni kikao kidogo cha kikatiba ambacho huwakinapisha bajeti ya shirikisho.


Amesema TUCTA inaahidi kuendelea kumpa ushirikiano Rais Samia na wanaamini katika sherehe za mei mosi za mwaka huu atafanya kitu kwa wafanyakazi,


“watumishi wa umma wanakilio kikubwa dhidi ya wakuu wa mikoa na wilaya kuwa na tabia ya kuwasweka lupango watumishi jambo ambalolimetusikitisha sana kila wilaya unayoenda unakutana na watumishi 10 u 20 wako ndani,”amesema


Naye Mwenyekiti wa kamati ya wanawake Tucta Rehema Ludanga alisema wafanyakazi wanazidi kujenga imani kwa serikali yao kwa kushirikiana na vyama vya wafanyakazi katika changamoto mbalimbali.


Amesema serikali inaona na kutambua kilio cha wafanyakazi na katika kuelekea siku ya wafanyakazi wanatarajia kusikia mambo mema na mazuri kutoka kwa serikali iliyoahidi.


“Natumia fursa hii kuwahasasa wafanyakazi wenzangu kufanya kazi kwa bidii ili iwe rahisi kwa serikali kuangalia namna bora ya kuboresha maslahi yetu na kikubwa tuchape kazi,”’amesema

Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI