Na Fatma Ally MDTV Dar es Salaam
Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM imeilekeza Serikali kuangalia upya mwenendo wa jeshi la Polisi nchini Tanzania ambao umekua hauridhishi kutokana na kulalamikiwa na wananchi kutokana na matendo yanayofanywa na baadhi ya maofisa na askari wa jeshi hilo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na uenezi Shaka Hamdu Shaka wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema jeshi hilo limekua likifanya matendo kinyume na muongozo wa utendaji wa kazi wa jeshi la Polisi (PGO).
Hatu hiyo imekuja baada ya kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi kuketi siku ya ijumaa Mach 11,2022 chini ya Mwenyekiti a chama hicho Rais Samia Suluhu ikulu chamwino jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine kamati imepokea taarifa kutoka vitengo vya idara za chama.
Aidha, kamati hiyo imempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kuunda tume kufuatilia matukio mbalimbali ya uhalifu na kupelekea baadhi ya watanzania kuuwawa katika mkoa ya Mtwara na Tanga wilaya ya Kilindi.
Katika hatua nyengine kamati hiyo imeridhia na kuelekeza kufanyika kwa mdahalo wa kitaifa ambao utakumbushia mema na mazuri yake kwa kuzingatia tulipotoka, tulipo na tunapokwenda.
Aidha kamati hiyo imepitisha mpango wa Chama Cha Mapinduzi kuhusu maadhimisho ya kumbukizi ya kitaifa ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa baba wa Taifa Hayyat Mwalim Julius Nyerere, ambapo mdahalo huo jumamosi April 9, 2022 katika shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere kibaha.
"Mdahalo huo utahudhuriwa na wanazuoni wabobezi wa masuala ya siasa, uchumi, uongozi na utawala, baadhi ya watu mashuhuri waliofanya kazi Mwalimu Nyerere , viongozi na watendaji wa Serikali, Taasisi za elimu ya juu pamoja Taasisi za fedha na mashirika yasio ya kiserikali"amesema Shaka.
Katika hatua nyengine, kamati hiyo imepitisha mapendekezo ya marekebisho ya katiba ya CCM 1977, toleo la 2020 huku ikiwa lengo kuu la marekebisho hayo ikiwa kuongeza ufanisi wa kazi za chama na utekelezaji wa maamuzi ya vikao vya chama.
"Malengo mengine ni pamoja na kuimarisha nguvu za chama katika kukabiliana na kudhibiti vitendo ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kukiwezesha chama kuwa imara"amesema Shaka
0 Comments