Header Ads Widget

WAZAZI WALEZI WATAKIWA KUTOA ELIMU KWA WATOTO JUU YA AFYA YA AKILI

 



Na Hamida Ramadhani Dodoma 


WAZAZI na Walezi wametakiwa kuwafundisha na kutoa elimu kwa watoto juu ya afya ya akili jambo litakalo wasaidia watoto au vijana kutougua ugonjwa wa akili na taifa la Tanzania kuwa na nguvukazi ya kutosha.


Akiongea na kituo hiki Mkurugenzi wa Peter's Daughters Initiative Doreen Noni amesema wazazi na walezi wamekuwa wakiwafundisha watoto wao kula vizuri huku wakisahau kutoa elimu juu ya afya ya akili .


" Hili lipo wazi vijana wamekuwa wakikubwa na tatizo la afya ya akili  na wahanga wakubwa wa tatizo hilo ni wale vijana balehe ambapo wengi wamekuwa wakipata tatizo hili huku wengine wakiishia kurukwa na akili na wengine wakiishia kupoteza uhai wao kwa kujiua," amesema Mkurugenzi huyo Doreen.


Na kuongeza kusema "Na Ndio maana sisi Peters Daughter Initiative tumeona tukutane na watoto au vijana hawa  katika jukwaa hili la hadithi hadithi jukwaa liliopambwa na burudani  mbalimbali ikiwemo nyimbo na maigizo kwa vijana lengo ni kuwapa nafasi kuja kuadithia kusikiliza kutoa elimu na kupata elimu kwa ujumla,"amesema 


Awali akiongea kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka katika jukwaa hilo Mkuu wa wilaya ya Kongwa Remidius mwema amesema mtu yoyote anaweza kukumbwa na tatizo la ugonjwa wa afya ya akili hivyo kama wazazi  tuhakikishe tunawalinda na kuwatunza vijana wetu ambao ndio taifa la kesho .


" Tunapopaza sauti basi elimu inawafikia watoto wengi zaidi  na jambo hili mlilolifanya nyinyi wana Peters Daughter Initiative ni mfano mzuri wa kuigwa na majukwaa kama haya ingependeza ifike hadi mashuleni kwani tumeshuhudia mauaji ya hovyo yakitokea katika nchi yetu watoto kuwaua wazazi wao na wengine kuuana kwa visasi vyote hivyo vinatokana na matatizo ya akili maana mtu mwenye akili sawasawa hawezi kumfanyia mwenzie unyama ," 


Kwa upande wake Dkt Omary Ubuguyu Mkurugenzi wa huduma na tiba kutoka wizara ya afya amesema matatizo ya afya ya akili yanaweza kumpata mtu yoyote hivyo vijana wanatakiwa kuwa na ujasiri wa kuzungumza hisia zao.


" Changamoto kubwa inayowakubwa vijana ni pamoja asilimia kubwa ya vijana kutokuwa na uelewa  juu ya afya ya  akili hali inayopelekea vijana wengi kuishia kujiua na wengine kuwaua wenzao," amesema Dkt Ubuguyu.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI