Na Mwandishi wetu, Mtwara
Baadhi ya wanufaika wa kaya masikini Wilayani Tandahimba mkoani Mtwara wamesema kuwa wameweza kufanya uwekezaji mdogo kupitia mashamba ili waweze kujikwamua kiuchumi ambapo katika msimu wa korosho uliopita walifanikiwa kupata kilo 50 za korosho ghafi.
Akizungumza mbele ya viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Ashura Ahmad Mlengwa kutoka Kijiji cha Madaba alisema kuwa waliwekeza kwenye korosho ambapo walipata shamba lenye mikorosho 20 ambalo walihudumia na kupata kiasi cha kilo 50 ambazo wanajipanga kubangua.
Alisema kuwa wazo la ubanguaji wa korosho hizo umekuba baada ya kuona bei ya korosho ghafi kuwa ndogo hivyo kuloazimika kujifunza ubanguaji ili waweze kuapata faida.
“Unajua sisi kama kikundi hatuna shamba ila tuna kikoba ambacho kina pesa mtu akihitaji mkopo tuna mpa bila riba lakini anawekeza kwetu kitu kama shamba au mali nyingine ambayo tunaweza kuitumia katika kipindi ambacho hajarejesha mkopo na ikatupa faida kubwa ingawa hata sisi tunakopeshana pia”
Hata hivyo Mratibu wa TASAF Wilaya ya Tandahimba Ismaely Mbilinyi anasema kuwa pesa za walengwa zimekuwa zikichelewa hivyo uwepo wa vikoba umewezesha wanakaya masikini kukopa na kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo.
“Walengwa wengi wanania ya kujikwamua kiuchumi ndio maana tunawapa miradi ya muda lakini pia wao wenyewe wamekuwa wakifanya miradi yao na ya vikundi ili kuwasadia kuendesha maisha ya kila siku”
“Mfano tukiwalipa sasa tunakuwa tumelipa mwezi wa 11 na 12 tu ndio maana vipo vikundi ambavyo vimesimama kufanya vikoba na miradi midogo midogo kwa kukosa ruzuku” alisema Mbilinyi
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Issa Naumanga alisema kuwa tunaunga mkono vikundi vya wanufaika wa mpango masikini ambao tunaamini kuwa wanafanya vizurii.
“Unajua kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini tumeona mafanikio makubwa katika Wilaya yetu pamoja na pesa kutolewa kidogo lakini ubunifu wa wanufaika umeonyesha kuwa hakuna linaloshindikana yaani wametuhamasisha hata kwenye mikopo tunawafikiria”
“Wananchi wengi walioingia katika mpango huu uwezo wao ni mdogo wanasaidiwa na mfuko huu lakini wanajiiongeza na kufanya makubwa zaidi bila kujali kiasi ambacho wanapokea lakini wanaunda umoja ambao unaonyesha kuwa na mafanikio makubwa zaidi” alisema Naumanga
MWISHO
0 Comments